01-Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An’aam: Kutokumshirikisha Allaah

 

Wasiya Kumi Katika Mwisho Wa Suwrah Al-An’aam

 

01-Kutokumshirikisha Allaah

 

 

 

 

 

 Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٥١﴾

Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao. Na wala msikaribie machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya shariy’ah). Hivyo ndivyo Alivyokuusieni  kwayo mpate kutia akilini.”

 

 

وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۖ وَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ بِالْقِسْطِ ۖ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَإِذَا قُلْتُمْ فَاعْدِلُوا وَلَوْ كَانَ ذَا قُرْبَىٰ ۖ وَبِعَهْدِ اللَّـهِ أَوْفُوا ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ ﴿١٥٢﴾

 “Na wala msiikaribie mali ya yatima isipokuwa kwa njia ya ihsaan mpaka afikie umri wa kupevuka. Na timizeni kipimo na mizani kwa uadilifu. Hatukalifishi nafsi isipokuwa kadiri ya uwezo wake. Na mnaposema basi fanyeni uadilifu japokuwa ni jamaa wa karibu. Na timizeni ahadi ya Allaah. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kukumbuka.”

 

 

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ﴿١٥٣﴾

 “Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.” [Al-An’aam: 151-153].

 

 

Wasiya uliokusudiwa katika Aayah hizo ni miongoni mwa maamrisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Hizi ni amri kumi zilokusanyika pamoja katika Suwrah hiyo tukufu ya Al-An’aam, lakini maamrisho kama hayo na mengineyo yametajwa pia katika Suwrah nyenginezo mbali mbali na katika Aayah mbali mbali kwenye Qur-aan.

 

Maamrisho kama hayo  yanafanana na maamrisho ya Allaah ('Azza wa Jalla) kwa  Ahlul-Kitaab (Mayahudi na Manaswara) kwani wao pia wameamrishwa mema na kuharamishwa maovu.   Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

Sema: “Enyi Ahlal-Kitaabi! Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa miola badala ya Allaah.” Wakikengeuka; basi semeni: “Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu.” [Aal-‘Imraan: 64]

 

 

Wasiya Wa Kwanza: Kutokumshirikisha Allaah ('Azza wa Jalla):

 

Anasema Allaah:

 

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا

Sema: “Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote, [Al-An’aam: 151]

 

 

Shirki ni dhambi pekee ambayo Allaah ('Azza wa Jalla) Hamsamehe mtu ikiwa hakutubia kama Anavyosema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

 إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدِ افْتَرَىٰ إِثْمًا عَظِيمًا ﴿٤٨﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amezua dhambi kuu. [An-Nisaa: 48]

 

Na kauli Yake Allaah ('Azza wa Jalla) nyengineyo kama hiyo:

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ ۚ وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا بَعِيدًا﴿١١٦﴾

Hakika Allaah Haghufurii kushirikishwa; lakini Anaghufuria yasiyokuwa hayo kwa Amtakae. Na yeyote atakayemshirikisha Allaah basi kwa yakini amepotoka upotofu wa mbali.  [An-Nisaa: 116]

 

 

Shirki ni katika dhambi kubwa mno na  inamuangamiza mtu:

 

Amesema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

 

((ألاَ أُنبِّئكم بأكبرِ الكبائر؟ الإشراك بالله)) متفق عليه.

((Je, hivi nikujulisheni madhambi makubwa kabisa? Ni kumshirikisha Allaah)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه (عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ)) قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَمَا هُنَّ؟  قَالَ: ((الشِّرْكُ بِاللَّهِ وَالسِّحْرُ وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلاَّ بِالْحَقِّ وَأَكْلُ الرِّبَا وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافلاَتِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jiepusheni na mambo saba yanayoangamiza!)) Wakauliza: Ni yepi hayo ee Rasuli wa Allaah? Akawaambia: ((Ni kumshirikisha Allaah, sihri [uchawi], kuua nafsi Aliyoiharamisha Allaah isipokuwa kwa haki, kula ribaa, kula mali ya yatima, kukimbia wakati wa vita na kuwatuhumu uzinifu wanawake Waumini waliohifadhika walioghafilika.)) [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Mwenye kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) hatoingia Jannah bali makazi yake yatakuwa ni motoni. Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

إِنَّهُ مَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّـهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ﴿٧٢﴾

 Hakika mwenye kumshirikisha Allaah bila shaka Allaah Atamharamishia Jannah, na makazi yake yatakuwa ni motoni. Na madhalimu hawatopata yeyote mwenye kunusuru.” [Al-Maaidah: 72]

 

Na Hadiyth kadhaa zimethibitisha, chache miongoni mwazo ni zifuatazo:

 

 

أَبِي ذَرّ رَضِيَ اللَّه عَنْهُ قَالَ : قَالَ رَسُول اللَّه صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  ((أَتَانِي جِبْرِيل فَبَشَّرَنِي أَنَّهُ مَنْ مَاتَ لَا يُشْرِك بِاَللَّهِ شَيْئًا مِنْ أُمَّتك دَخَلَ الْجَنَّة قُلْت وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ قُلْت وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ قُلْت وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ ؟ قَالَ وَإِنْ زَنَى وَإِنْ سَرَقَ وَإِنْ شَرِبَ الْخَمْر))متفق عقيه

 

Kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah  (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Amenijia Jibriyl akanibashiria kwamba yeyote katika Ummah wangu atakayefariki akiwa hakumshirikisha Allaah na chochote, ataingia Peponi. Nikasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba? Akasema: Hata kama ikiwa amezini na ameiba. Nikasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba? Akasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba. Nikasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba?  Akasema: Hata ikiwa amezini na ikiwa ameiba na ikiwa amekunywa pombe)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Pia:

 

 عن جابر رضي الله عنه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: ((مَنْ لَقِي اللهَ لاَ يُشْرِك بِهِ شَيْئاً دَخَلَ الْجَنَّة، وَمَنْ لَقِيَه يُشْرِك بِهِ شَيْئاً دَخَلَ النَّار)) 

Imetoka kwa Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (Atakayekutana na Allaah akiwa hamshirikishi na chochote Ataingia Jannah, na atakayekutana Naye akiwa anamshirikisha na chochote ataingia Motoni)) [Muslim 94.]

 

 

Na:

 

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: (( مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللهِ نِدَّاً دَخَلَ النَّارَ )) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaahi bin Mas-‘uwd (Radhwiya Alaahu ‘anhu) amesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayekufa akiwa katika hali ya kumuomba asiyekuwa Allaah kumfanyia mlinganishi (mshirika) ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

عن ابن مسعود رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللَّهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ))  

Kutoka kwa Ibn Mas‘uwd pia kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayefariki akiwa katika hali ya kumshirikisha Allaah kwa chochote ataingia Motoni)) [Al-Bukhaariy 1238, Muslim 92]

 

Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada na bayana kabisa kuhusiana na shirki:

 

 

إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ --- Hakika Shirki Ni Dhulma Kubwa Mno!

 

 

 

  

 

Share