Al-Lajnah Ad-Daaimah: Kutawassal Kwa Walio Makaburini Haijuzu Kwani Hawasikii Sauti Za Wanaowaomba
Kutawassal Kwa Waliofariki Makaburini Haijuzu Kwani Hawasikii Sauti Za Wanaowaomba
Al-Lajnah Ad-Daaimah:
‘Ulamaa wa Al-Lajnah Ad-Daaimah wamesema:
“Akishafariki mwana Aadam, masikio yake hayafanyi kazi wala hadiriki kusikia sauti za duniani wala kusikia maongezi yao kwani Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
وَمَا أَنتَ بِمُسْمِعٍ مَّن فِي الْقُبُورِ ﴿٢٢﴾
nawe huwezi kuwasikilizisha walioko kaburini. [Faatwir: 22]
[Fataawa Al-Lajnah Ad-Daaimah (1/478-479)]
