38-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah: Atakayesema AstaghfiruAllaahAlladhiy Laa Ilaaha Illa Huwa …. Atamghfuria Hata Kama Ana Makosa Ya Kukimbia Vitani

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

38-Atakayesema AstaghfiruAllaahAlladhiy Laa Ilaaha Illa Huwa …. Atamghfuria Hata Kama Ana Makosa Ya Kukimbia Vitani 

 

 

 

عن بِلاَلَ بْنَ يَسَارِ بْنِ زَيْدٍ، مَوْلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ سَمِعْتُ أَبِي يُحَدِّثُنِيهِ عَنْ جَدِّي أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: (( مَنْ قَالَ أَسْتَغْفِرُ اللَّهَ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ الْحَىُّ الْقَيُّومُ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ غُفِرَ لَهُ وَإِنْ كَانَ فَرَّ مِنَ الزَّحْفِ ))

 

Imepokelewa kutoka kwa Bilaal bin Yasaar bin Zayd mkombolewa wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba nimesikia baba yangu amenihadithia kutoka kwa babu yangu kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ’alayhi wa aalihi wa sallam amesema: ((Atakayesema:

أَسْتَغْفِرُ اللهَ الْعَظِيمَ الَّذِي لَا إِلَهَ إلَّا هُوَ الحَيُّ القَيّوُمُ وأَتُوبُ إِلَيهِ

Astaghfiru-Allaahal-‘Adhwiyma Alladhiy laa ilaaha illaa Huwal-Hayyul-Qayyuwmu wa atuwbu Ilayhi

 

Namuomba maghfira kwa Allaah Mtukufu Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu, na ninarejea kutubuia Kwake...

 

 Allaah Atamghufuria kama ana makosa hata kama ya kukimbia vitani)) [Abu Daawuwd (2/85) [1517], At-Tirmidhiy (5/569) [3577], Al-Haakim na ameisahihisha na ameikubali Adh-Dhahaby (1/511) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله). Angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/182)]

 

 

 

Share