39-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Du’aa Ya Swafaa Na Marwah Na Unaporudi Safarini

Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah

 

www.alhidaaya.com

 

39-Du’aa Ya Swafaa Na Marwah Na Unaporudi Safarini

 

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alisoma hivi mara tatu alipopanda jabali la Swafaa na baina yake akiomba du’aa, kisha akafanya alipokuwa Marwah kama alivyofanya alipokuwa Swafaa:

 

لا إِلهَ إلاَّ  اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ وهُوَ عَلى كُلِّ شَيءٍ قَديرٌ، لا إِلَهَ إلا اللهُ وَحْدَهُ أَنْجَزَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ

Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul  Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu, Anjaza wa’dahu, Wa naswara ’abdahu,  wa hazamal ahzaaba Wahdah

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na Himdi Anastahiki Yeye, Naye juu ya kila kitu ni Muweza. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake, Ametekeleza ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake. [Muslim (2/888) [1218]

 

Pia:

 

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رضى الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا قَفَلَ مِنْ غَزْوٍ أَوْ حَجٍّ أَوْ عُمْرَةٍ يُكَبِّرُ عَلَى كُلِّ شَرَفٍ مِنَ الأَرْضِ ثَلاَثَ تَكْبِيرَاتٍ، ثُمَّ يَقُولُ:  لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَ عَابِدُونَ سَاجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُ وَعْدَهُ وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ ‏

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullah bin ‘Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anaporudi vitani au Hajj au ‘Umrah kila alipopanda mnyanyuko wa ardhi alileta Takbiyrah (Allaahu Akbar) mara tatu  kisha akisema:

 

 لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ، وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، آيِبُونَ تَائِبُونَ عَابِدُونَ سَاجِدُونَ لِرَبِّنَا حَامِدُونَ، صَدَقَ اللَّهُ وَعْدَهُ وَنَصَرَ عَبْدَهُ وَهَزَمَ الأَحْزَابَ وَحْدَهُ ‏ 

Laa ilaaha illa Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahu mulku walahul  Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr.  Aayibuwna, taaibuwna, ‘aabiduwnaa, saajiduwna, li-Rabbinaa haamiduwna. Swadaqa Allaahu Wa’dahu, wa-Naswara ’Abdahu wa-Hazama Al-Ahzaaba Wahdahu

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kuwa Peke Yake, wala hana mshirika. Ni wake ufalme na Himdi Anastahiki Yeye, Naye juu ya kila kitu ni MuwezaTunarudi hali ya kuwa tunatubia, tunaabudu, tunasujudu na Rabb wetu tunamsifu. Amesadikisha ahadi Yake, na Amemnusuru mja Wake, na Amevishinda vikosi Peke Yake. [Al-Bukhaariy na wengineo]

 

 

Share