40-Fadhila Za Laa Ilaaha Illa-Allaah: Du’aa Ya Kuogopa Ukandamizaji Na Dhulma Ya Mtawala: Allaahumma Rabbas-Samaawatis-Sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwim...
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah
40-Du’aa Ya Kuogopa Ukandamizaji Na Dhulma Ya Mtawala: Allaahumma Rabbas-Samaawatis-Sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwim...
عن عبدِ اللَّهِ بنِ مسعودٍ إذا كانَ على أحدِكم إمامٌ يخافُ تَغطرُسَهُ أو ظلمَهُ فليقلِ
Athar ya ‘Abdullaah bin Mas’uwd (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: “Ikiwa kuna aliye na madaraka nawe ambaye unaogopa ukandamizaji wake na dhulma yake, basi aseme:
أللَّهُمَّ رَبَّ السَّمواتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيم، كُنْ لِي جاَراً مِنْ (فُلانِ بْنِ فُلاَنٍ) وَأَحْزَابِهِ مِنْ خَلاَئِقِكَ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيَّ أحَدٌ مِنْهُمْ أَوْ يَطْغَى، عَزَّ جاَرُكَ وَجَلَّ ثَناَؤُكَ، وَ لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ
Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwim, kun liy jaaran min (fulani bin fulani) wa ahzaabihi min Khalaaiqika an yafrutwa ‘alayya ahadun minhum aw yatw-ghaa. ‘Azza Jaaruka, wa Jalla Thanaauka, walaa ilaaha illaa Anta
Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arshi Tukufu, kuwa Mlinzi wangu kutokana na (fulani bin fulani [taja mtu unayemkhofu]) na vikosi vyake miongoni mwa viumbe Vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni mwao, au kunifanyia uadui. Imeimarika madhubuti hifadhi Yako, na zimetukuka sifa Zako na hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe.
[Al-Bukhaariy Al-Adab Al-Mufrad [707] na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [545, 546].