05-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango wa As-Salam (Malipo Ya Kabla), Kukopesha Na Kuweka Rahani
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْبُيُوعِ
Kitabu Cha Biashara
أَبْوَابُ اَلسَّلَمِ وَالْقَرْضِ، وَالرَّهْنِ
05-Mlango wa As-Salam (Malipo Ya Kabla),[1] Kukopesha[2] Na Kuweka Rahani
719.
عَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَدِمَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ اَلْمَدِينَةَ، وَهُمْ يُسْلِفُونَ فِي اَلثِّمَارِ اَلسَّنَةَ وَالسَّنَتَيْنِ، فَقَالَ: {مَنْ أَسْلَفَ فِي تَمْرٍ فَلْيُسْلِفْ فِي كَيْلٍ مَعْلُومٍ، وَوَزْنٍ مَعْلُومٍ، إِلَى أَجَلٍ مَعْلُومٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ.
وَلِلْبُخَارِيِّ: "مَنْ أَسْلَفَ فِي شَيْءٍ"
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliingia Madiynah na wao (wenyeji) wanafanya salaf katika matunda; kwa mwaka mmoja na miaka miwili. Akasema: “Atakayefanya salaf katika matunda basi afanye katika kipimo maalumu, na wizani maalumu na kwa muda maalumu.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah ya Al-Bukhaariy imesema: “Atakayefanya salaf katika kitu chochote…”
720.
وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ أَبْزَى، وَعَبْدِ اَللَّهِ بْنِ أَبِي أَوْفَى رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَا: {كُنَّا نُصِيبُ اَلْمَغَانِمَ مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ وَكَانَ يَأْتِينَا أَنْبَاطٌ مِنْ أَنْبَاطِ اَلشَّامِ، فَنُسْلِفُهُمْ فِي اَلْحِنْطَةِ وَالشَّعِيرِ وَالزَّبِيبِ وَفِي رِوَايَةٍ: وَالزَّيْتِ إِلَى أَجَلٍ مُسَمًّى. قِيلَ: أَكَانَ لَهُمْ زَرْعٌ ؟ قَالَا: مَا كُنَّا نَسْأَلُهُمْ عَنْ ذَلِكَ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa ‘Abdul-Rahmaan bin Abzaa[3] na ‘Abdullaah bin Abiy Awfaa (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) wamesema: “Tulikuwa tukipata ghanima pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na tulikuwa tukijiliwa na Anbaatw[4] wa Sham (Syria, Palestina, Lebanon na Jordan) tulikuwa tukiwalipa kabla kwa ngano, shayiri[5] na zabibu.
Katika Riwaayah nyingine inasema: …na zeti (ya Zaituni) kwa muda maalumu. Wakasema: Walikuwa na mazao? Akasema: Hatukuwa tukiwauliza swala hilo.”[6] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
721.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {مَنْ أَخَذَ أَمْوَالَ اَلنَّاسِ يُرِيدُ أَدَاءَهَا، أَدَّى اَللَّهُ عَنْهُ، وَمَنْ أَخَذَهَا يُرِيدُ إِتْلَافَهَا، أَتْلَفَهُ اَللَّهُ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye kuchukua mali ya watu anakusudia kuilipa, Allaah atamuwezesha kulipa. Na mwenye kuichukua kwa niyyah ya kuiharibu Allaah Atamuangamiza.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
722.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: {قُلْتُ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ ! إِنَّ فُلَاناً قَدِمَ لَهُ بَزٌّ مِنَ اَلشَّامِ، فَلَوْ بَعَثْتَ إِلَيْهِ، فَأَخَذْتَ مِنْهُ ثَوْبَيْنِ بِنَسِيئَةٍ إِلَى مَيْسَرَةٍ؟ فَأَرْسَلَ إِلَيْهِ، فَامْتَنَعَ} أَخْرَجَهُ اَلْحَاكِمُ، وَالْبَيْهَقِيُّ، وَرِجَالُهُ ثِقَاتٌ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema: “Nilisema: Ee Rasuli wa Allaah! Fulani amekuja na nguo kutoka Sham, waonaje lau ungelimtuma mtu ukachukua kwake nguo mbili kwa mkopo[7] hadi utakapopata? Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamtuma mtu, yule (muuzaji) akakataa.” [Imetolewa na Al-Haakim na Al-Bayhaqiyy. Wapokezi wake ni madhubuti]
723.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {اَلظَّهْرُ يُرْكَبُ بِنَفَقَتِهِ إِذَا كَانَ مَرْهُونًا، وَلَبَنُ اَلدَّرِّ يُشْرَبُ بِنَفَقَتِهِ إِذَا كَانَ مَرْهُونًا، وَعَلَى اَلَّذِي يَرْكَبُ وَيَشْرَبُ اَلنَّفَقَةُ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mnyama anapandwa kwa matumizi yake[8] kama mnyama amewekwa rahani[9] na maziwa yatanywewa kwa matumizi yake ikiwa amewekwa rahani, na anayepanda na kukamua ni juu yake matumizi.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
724.
وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: {لَا يَغْلَقُ اَلرَّهْنُ مِنْ صَاحِبِهِ اَلَّذِي رَهَنَهُ، لَهُ غُنْمُهُ، وَعَلَيْهِ غُرْمُهُ} رَوَاهُ اَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَالْحَاكِمُ، وَرِجَالهُ ثِقَاتٌ. إِلَّا أَنَّ اَلْمَحْفُوظَ عِنْدَ أَبِي دَاوُدَ وَغَيْرِهِ إِرْسَالُهُ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Rahani haitoki kwenye umiliki wa mwenyewe aliyeweka rahani, nyongeza yake ni yake, matumizi yake ni juu yake.”[10] [Imetolewa na Ad-Daaraqutwniyy na Al-Haakim. Wapokezi wake ni waaminifu (madhubuti)
725.
وَعَنْ أَبِي رَافِعٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ اسْتَسْلَفَ مِنْ رَجُلٍ بَكْرًا فَقَدِمَتْ عَلَيْهِ إِبِلٌ مِنَ اَلصَّدَقَةِ، فَأَمَرَ أَبَا رَافِعٍ أَنْ يَقْضِيَ اَلرَّجُلَ بَكْرَهُ، فَقَالَ: لَا أَجِدُ إِلَّا خَيَارًا قَالَ: " أَعْطِهِ إِيَّاهُ، فَإِنَّ خِيَارَ اَلنَّاسِ أَحْسَنُهُمْ قَضَاءً} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Abuu Raafi’ (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikopesha ndama wa ngamia kwa mtu. (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaletewa ngamia wa Swadaqah. Akamuamuru Abuu Raafi’ kumlipa yule ngamia wake. (Abuu Raafi’) akasema: Sina isipokuwa ngamia bora mwenye miaka saba. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Mpe huyo kwani ni mbora wao wa kulipa.”[11] [Imetolewa na Muslim]
726.
وَعَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ {كُلُّ قَرْضٍ جَرَّ مَنْفَعَةً، فَهُوَ رِبًا} رَوَاهُ اَلْحَارِثُ بْنُ أَبِي أُسَامَةَ، وَإِسْنَادُهُ سَاقِطٌ.
وَلَهُ شَاهِدٌ ضَعِيفٌ عَنْ فَضَالَةَ بْنِ عُبَيْدٍ عِنْدَ اَلْبَيْهَقِيِّ
وَآخَرُ مَوْقُوفٌ عَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ سَلَامٍ عِنْدَ اَلْبُخَارِيِّ
Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kila mkopo unaoleta manufaa hiyo ni ribaa.” [Imetolewa na Al-Haarith bin Abuu Usaamah na katika Isnaad yake kuna mtu ameachwa.
Al-Bayhaqiyy amepokea kama ni ushahidi mwingine ingawaje ni Hadiyth dhaifu kutoka kwa Fadhwaalah bin ‘Ubayd.
Al-Bukhaariy ameipokea ikiwa ni Mawquwf kutoka kwa ‘Abdullaah bin Salaam.
[1] Salam ina maana ya kununua kitakachozalishwa kwa malipo ya kabla. Kwa mfano mtu anampa mtu mwingine fedha na kumuambia kuwa atampa kitu chenyewe muda fulani kwa bei kadhaa. Hili linaruhusiwa maadamu kuwa bei na thamani yake imekubaliwa hapo kabla. Kwa lugha nyingine inaitwa Salaf.
[2] Kukopesha kwa kiarabu imeitwa Qardhw, ambapo maana yake ni kukata kitu. Mtu anayemkopesha mwenziwe pesa huwa anakata katika zile pesa zake na kumpatia yule anayemkopesha. Katika shariy’ah kukopesha (Qardhw) ni kumpa mtu pesa ambazo zitamsaidia, na mtu huyo anatakiwa kulipa kiwango kile kile alichopewa hapo awali bila ya nyongeza yoyote.
[3] ‘Abdul-Rahmaan bin Abzaa Al-Khuzaa’iy, ni muachwa huru wa Banuw Khuzaa’ alikuwa ni Swahaba mdogo kwa umri ambaye aliwahi kuswali nyuma ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Aliishi Al-Kufah (‘Iraaq), na ‘Aliy bin Abiy Twaalib alimfanya kuwa gavana wa Khurasaan. Alifariki Kufa.
[4] Anbaatw ni warabu waliohamia katika miji wa Waajemi na Warumi wakachanganyikana nao.
[5] Shayiri: nafaka inayofanana na ngano inayotumika kuwa chakula.
[6] Hadiyth hii inajuzisha Bayi’ As-Salam hata kama mazao hayakuwepo wakati wa mauzo. Cha msingi ni kuwa mazao yawe tayari kwa wakati ule.
[7] Ina maana kuwa kununua kitu kwa mkopo inaruhusiwa. Muuza nguo alikuwa ni Yahudi na alikuwa na uadui na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), na ndio maana alikataa.
[8] Ina maana ikiwa mtu ameweka rahani farasi au ng’ombe wake kwa mkopo aliochukua. Kuna tafsiri ya aina mbili: Ima mkopeshaji atamlisha farasi au ng’ombe na akafaidika nao au mkopaji atamlisha farasi au ng’ombe akafaidika nao. Yeyote atakayewalisha ndio anayestahiki maslahi yao. Hadiyth hii inathibitisha muono wa pili.
[9] Kulingana na Shariy’ah, rahani ni kutoa aina ya miliki au kitu cha anayekopa kama dhamana ya mkopo anaouchukua.
[10] Hii ina maana aliyepewa dhamana si mmiliki wa rahani iliyo kwake. Anaidhibiti tu. Ikiwa rahani imeharibika au kufa, aliyepewa dhamana hana majukumu ya kulipa. Vivyo hivyo kama kutakuwa na ziada ya rahani iliyoongezeka hatokuwa mmiliki wake. Hasara na faida, vyovyote ilivyo inakwenda kwa mmiliki na sio kwa aliyewekewa rahani. Hali hii imebatilisha hali ya kijahiliya ya hapo kabla. Waarabu hapo zamani walikuwa wakiwekeana rahani, yule muweka rahani anaposhindwa kulipa kile kitu chake kinachukuliwa na yule ambaye rahani iko kwake. Iwapo kilichowekwa rahani ni kitu kama matunda au mtoto, basi yule aliyeweka rahani ndiye anayelazimika kusimamia matumizi ya alichoweka rahani ili kiendelee kuishi.
[11] Ikiwa mdaiwa ametoa faida aliyoipata pamoja na ile fedha aliyokopa si vibaya ni halali kwa mkopeshaji kuchukua. Ama ikiwa mkopeshaji ameweka sharti mkopo urejeshwe na ziada inachukuliwa kama ribaa nayo ni haraam. Kurudisha kilichokua kizuri inaruhusiwa na ni halali kwa mkopeshaji lakini ikilazimishwa kurejesha ziada pamoja na mali aliyokopa ni ribaa na ni haraam. Hadiyth hii yaonesha tabia njema na huwa haihesabiwi kuwa ni mkopo wenye nyongeza, kwa sababu wakati wa kutolewa haukuwa umewekewa sharti. Ni mwenyewe aliyekopa kwa furaha yake anamtunukia zawadi mkopeshaji.