04-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Ruhusa Katika ‘Araayaa Na Kuuza Mashina Na Matunda
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلْبُيُوعِ
Kitabu Cha Biashara
بَابُ اَلرُّخْصَةِ فِي اَلْعَرَايَا وَبَيْعِ اَلْأُصُولِ وَالثِّمَارِ
04-Mlango Wa Ruhusa Katika ‘Araayaa Na Kuuza Mashina Na Matunda
712.
عَنْ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {رَخَّصَ فِي اَلْعَرَايَا: أَنْ تُبَاعَ بِخَرْصِهَا كَيْلاً} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَلِمُسْلِمٍ:{رَخَّصَ فِي اَلْعَرِيَّةِ يَأْخُذُهَا أَهْلُ اَلْبَيْتِ بِخَرْصِهَا تَمْرًا، يَأْكُلُونَهَا رُطَبًا}
Kutoka kwa Zayd bin Thaabit (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ): “Ameruhusu katika ‘Aryaaaa[1] ziuzwe kwa kuzikadiria kwa kipimo.” [Al-Bukaariy, Muslim]
Na katika Muslim imesema: “Ameruhusu katika ‘Ariyyah watu wa nyumbani wanazichukua kwa kuzikadiria na tende, na wale zilizoiva zikichumwa kutoka mtini.”
713.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ رَخَّصَ فِي بَيْعِ اَلْعَرَايَا بِخَرْصِهَا، فِيمَا دُونَ خَمْسَةِ أَوْسُقٍ، أَوْ فِي خَمْسَةِ أَوْسُقٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliruhusu katika biashara ya ‘Araayaa kwa kuzikadiria na tende chini ya wasaqi[2] tano au wasaqi tano.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
714.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَهَى رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ بَيْعِ اَلثِّمَارِ حَتَّى يَبْدُوَ صَلَاحُهَا، نَهَى اَلْبَائِعَ وَالْمُبْتَاعَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ:{وَكَانَ إِذَا سُئِلَ عَنْ صَلَاحِهَا ؟ قَالَ: "حَتَّى تَذْهَبَ عَاهَتُهُ "}
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuza matunda hadi yamedhihiri kufaa kwake, amemkataza muuzaji na mnunuzi.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
Na katika Riwaayah nyingine imesema: “Na alikuwa anapoulizwa kuhusu kufaa kwake husema: mpaka iondoke aibu yake.”[3]
715.
وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ بَيْعِ اَلثِّمَارِ حَتَّى تُزْهَى. قِيلَ: وَمَا زَهْوُهَا ؟ قَالَ: " تَحْمَارُّ وَتَصْفَارُّ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ ، وَاللَّفْظُ لِلْبُخَارِيِّ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuza matunda mpaka yapevuke. Wakasema: Kupevuka kwake ni vipi? Akasema: Mpaka yawe mekundu au manjano.” [Al-Bukhaariy, Muslim na tamshi hili ni la[4] Al-Bukhaariy]
716.
وَعَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ { أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ نَهَى عَنْ بَيْعِ اَلْعِنَبِ حَتَّى يَسْوَدَّ، وَعَنْ بَيْعِ اَلْحَبِّ حَتَّى يَشْتَدَّ} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ، إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ
Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza kuuza zabibu mpaka iwe nyeusi na amekataza kuuza nafaka mpaka iwe ngumu.”[5] [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim]
717.
وَعَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَوْ بِعْتَ مِنْ أَخِيكَ ثَمَراً فَأَصَابَتْهُ جَائِحَةٌ، فَلَا يَحِلُّ لَكَ أَنْ تَأْخُذَ مِنْهُ شَيْئًا. بِمَ تَأْخُذُ مَالَ أَخِيكَ بِغَيْرِ حَقٍّ ؟} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ:{أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَمَرَ بِوَضْعِ اَلْجَوَائِحِ}
Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Lau utamuuzia nduguyo matunda na yakapatwa na maafa basi si halali kwako kuchukua kitu kutoka kwake.[6] Kwa nini uchukue mali ya nduguyo bila haki?” [Imetolewa na Muslim]
Na katika Riwaayah yake nyingine amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameamrisha kutupiliwa mbali malipo ya matunda yaliyopata maafa.”[7]
718.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {مَنِ اِبْتَاعَ نَخْلًا بَعْدَ أَنْ تُؤَبَّرَ، فَثَمَرَتُهَا لِلْبَائِعِ اَلَّذِي بَاعَهَا، إِلَّا أَنْ يَشْتَرِطَ اَلْمُبْتَاعُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Atakayenunua mtende baada ya uchavushi,[8] basi matunda yake ni ya aliyeuza isipokuwa mnunuzi atakaposhurutisha.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
[1] ‘Araayaa (wingi wa ‘Ariyyah) ni mtu kumzawadia maskini tende zake zinazokadiriwa wasaqi tano (kapu tano sawa na kilo 715 takriban) kisha yule mwenye shamba akaona uzito yule maskini kuingia katika shamba lake kwenda kuchuma basi akazinunua kwa kuzikadiria na tende kavu.
[2] Kipimo cha Wasaqi tano: hukisiwa kuwa ni kilo 650 takriban.
[3] Neno la kiarabu ‘Aahat lina maana ya magonjwa ya ghafla, aina hii ya biashara inakatazwa kwa sababu matunda ambao hayajawiva hayafai na matumizi yake si sawa, huenda ugonjwa ukayaangukia na kuyaharibu kwa kuyateketeza. Kwa uwezekano huu wa kuharibika ndio maana ukakatazwa kwa lugha nyingine yasiwe na baka: maradhi ya mimea.
[4] Hadiyth yamalizika hivi: Akasema: “(Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) Waonaje Allaah Akizuia (kuosha), matunda ni kwa kitu gani mmoja wenu atahalalisha mali ya nduguye?”
[5] Ina maana hadi ikomae, ndipo inaporuhusiwa kuuzwa. Hadiyth yaonyesha kuwa kuwiva kwa zabibu ni kuwa nyeusi na kuwiva kwa nafaka ni kuwa ngumu. Kila chakula kina namna yake ya kuwiva.
[6] Kama matunda yapo mtini na yakapatwa na maafa, mwenye mti atahusika na hasara ile. Ikiwa maafa ni baada ya kuchumwa kwa matunda basi hasara itabebwa na mnunuzi.
[7] Neno la kiarabu وَضْعِ اَلْجَوَائِحِ ina maana hata baada ya kuyachuma yakaonekana ambayo yameharibika muuzaji anatakiwa ampunguzie mteja wake.
[8] Uchavushi ni kupandisha ni kupasua tawi la mtende jike na kupandikiza la mtende dume.