20-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Faraaidhw (Mafungu Ya Wanaorithi)

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ اَلْفَرَائِضِ

20-Mlango Wa Faraaidhw (Mafungu Ya Wanaorithi)[1]

 

 

 

 

 

 

805.

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {أَلْحِقُوا اَلْفَرَائِضَ بِأَهْلِهَا، فَمَا بَقِيَ فَهُوَ لِأَوْلَى رَجُلٍ ذَكَرٍ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

 Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wapeni mafungu wenye mafungu yao[2] kitakachobaki (baada ya kuwapa wenye mafungu yao) ni cha mwanamume aliye karibu zaidi (na maiti).” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

806.

وَعَنْ أُسَامَةَ بْنِ زَيْدٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: {لَا يَرِثُ اَلْمُسْلِمُ اَلْكَافِرَ، وَلَا يَرِثُ اَلْكَافِرُ اَلْمُسْلِمَ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ 

Kutoka kwa Usaamah bin Zayd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muislamu hamrithi kafiri wala kafiri hamrithi Muislamu.”[3] [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

807.

وَعَنْ اِبْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  فِي بِنْتٍ، وَبِنْتِ اِبْنٍ، وَأُخْتٍ { قَضَى اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ "لِلِابْنَةِ اَلنِّصْفَ، وَلِابْنَةِ اَلِابْنِ اَلسُّدُسَ تَكْمِلَةَ اَلثُّلُثَيْنِ وَمَا بَقِيَ فَلِلْأُخْتِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ

  Kutoka kwa Ibn Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesimulia katika kumrithisha binti, binti ya mtoto wa kiume na dada: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alihukumu binti apate nusu, binti ya mtoto wa kiume apate sudus kukamilisha thuluthi mbili[4] na kilichobakia ni cha dada.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]

 

 

 

808.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عَمْرٍو  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَا يَتَوَارَثُ أَهْلُ مِلَّتَيْنِ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ  وَأَخْرَجَهُ اَلْحَاكِمُ بِلَفْظِ أُسَامَةَ.  وَرَوَى النَّسَائِيُّ حَدِيثَ أُسَامَةَ بِهَذَا اَللَّفْظِ 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Wenye dini tofauti hawarithiani.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa At-Tirmidhiy, Al-Haakim ameipokea kwa maneno ya Usaamah; na An-Nasaaiy ameitaja Hadiyth ya Usaamah kwa tamshi hili]

 

 

 

809.

وَعَنْ عِمْرَانَ بْنِ حُصَينٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَقَالَ: {إِنَّ اِبْنَ اِبْنِي مَاتَ، فَمَا لِي مِنْ مِيرَاثِهِ؟ فَقَالَ: " لَكَ اَلسُّدُسُ " فَلَمَّا وَلَّى دَعَاهُ، فَقَالَ: "لَكَ سُدُسٌ آخَرُ" فَلَمَّا وَلَّى دَعَاهُ. فَقَالَ : "إِنَّ اَلسُّدُسَ اَلْآخَرَ طُعْمَةٌ} رَوَاهُ أَحْمَدُ وَالْأَرْبَعَةُ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ 

وَهُوَ مِنْ رِوَايَةِ اَلْحَسَنِ اَلْبَصْرِيِّ عَنْ عِمْرَانَ، وَقِيلَ : إِنَّهُ لَمْ يَسْمَعْ مِنْهُ

Kutoka kwa ‘Imraan bin Huswayn (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Mtoto wa mtoto wangu amefariki, nitapata nini katika mirathi yake? Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: Utapata sudusi. Alipogeuka alimuita akasema: Utapata sudusi nyingine.[5] Alipogeuka tena alimuita tena akasema: Ile sudusi nyingine ni ziada.”[6] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha At-Tirmidhiy]

Nayo ni katika Riwaayah ya Al-Hassan Al-Baswriyy[7] kutoka kwa ‘Imraan na inasemekana kuwa hajamsikia.

 

 

 

810.

وَعَنِ ابْنِ بُرَيْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ، {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  جَعَلَ لِلْجَدَّةِ اَلسُّدُسَ، إِذَا لَمْ يَكُنْ دُونَهَا أُمٌّ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ ، وَالنَّسَائِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ  ، وَقَوَّاهُ اِبْنُ عَدِيٍّ 

Kutoka kwa Ibn Buraydah naye kutoka kwa baba yake amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amempa bibi[8] sudusi iwapo hakuna mama pamoja naye.”[9] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na An-Nasaaiy, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah, Ibn Al-Jaaruwd na akaipa nguvu Abn ‘Adiyy

 

 

 

811.

وَعَنْ اَلْمِقْدَامِ بْنِ مَعْدِ يكَرِبَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {اَلْخَالُ وَارِثُ مَنْ لَا وَارِثَ لَهُ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ سِوَى اَلتِّرْمِذِيِّ، وَحَسَّنَهُ أَبُو زُرْعَةَ اَلرَّازِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ 

Kutoka kwa Al-Miqdaam bin Ma’d Yakrib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mjomba ni mrithi wa asiyekuwa na mrithi.”[10] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa At-Tirmidhiy, na Abuw Zur’ah Ar-Raaziy amesema ni Hasan, na akaisahihisha Ibn Hibbaan na Al-Haakim

 

 

 

812.

وَعَنْ أَبِي أُمَامَةَ بْنِ سَهْلٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {كَتَبَ مَعِي عُمَرُ إِلَى أَبِي عُبَيْدَةَ  رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمْ، أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  قَالَ: " اَللَّهُ وَرَسُولُهُ مَوْلَى مَنْ لَا مَوْلَى لَهُ، وَالْخَالُ وَارِثُ مَنْ لَا وَارِثَ لَهُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ سِوَى أَبِي دَاوُدَ، وَحَسَّنَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Abuu Umaamah bin Sahl[11] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “’Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alimuandikia barua Abuu ‘Ubaydah[12] kuwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: Allaah na Rasuli wa Allaah ni Wasimamizi wa asiyekuwa na msimamizi. Mjomba ni mrithi wa asiyekuwa na mrithi.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Ibn Maajah) isipokuwa Abuu Daawuwd, na At-Tirmidhiy amesema ni Hasan, na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

813.

وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {إِذَا اِسْتَهَلَّ اَلْمَوْلُودُ وُرِّثَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ 

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema “Mtoto aliyezaliwa akilia, anarithi.”[13] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na akaisahihisha Ibn Hibbaan]

 

 

 

814.

وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {لَيْسَ لِلْقَاتِلِ مِنَ الْمِيرَاثِ شَيْءٌ} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ، وَاَلدَّارَقُطْنِيُّ، وَقَوَّاهُ اِبْنُ عَبْدِ اَلْبَرِّ، وَأَعَلَّهُ النَّسَائِيُّ، وَالصَّوَابُ: وَقْفُهُ عَلَى عُمَرَ

Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Muuaji hana chochote katika mirathi.”[14] [Imetolewa na An-Nasaaiy, Ad-Daaraqutwniy na akaipa nguvu Ibn ‘Abdi-Barr, na akaidhoofisha An-Nasaaiy. Lakini sawa ni kuwa Hadiyth hii ni Mawquwf]

 

 

 

815.

وَعَنْ عُمَرَ بْنِ اَلْخَطَّابِ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  يَقُولُ:{مَا أَحْرَزَ اَلْوَالِدُ أَوْ اَلْوَلَدُ فَهُوَ لِعَصَبَتِهِ مَنْ كَانَ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَالنَّسَائِيُّ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ اَلْمَدِينِيِّ، وَابْنُ عَبْدِ اَلْبَرِّ

Kutoka kwa ‘Umar bin Al-Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akisema: “Anachochukua baba au mtoto (katika walaa) ni cha ‘Aswabah yake[15] yeyote awaye.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ibn Maajah, na akaisahihisha Ibn Al-Madiyniy na Ibn ‘Abdil-Barr]

 

 

 

816.

وَعَنْ عَبْدِ اَللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {اَلْوَلَاءُ لُحْمَةٌ كَلُحْمَةِ اَلنَّسَبِ، لَا يُبَاعُ، وَلَا يُوهَبُ} رَوَاهُ اَلْحَاكِمُ: مِنْ طَرِيقِ اَلشَّافِعِيِّ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ اَلْحَسَنِ، عَنْ أَبِي يُوسُفَ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ حِبَّانَ، وَأَعَلَّهُ اَلْبَيْهَقِيُّ 

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Walaa[16] ni udugu kama udugu wa nasaba, hauuzwi wala hautolewi hiba (zawadi).” [Imetolewa na Al-Haakim kwa njia ya Ash-Shaafi’iyy kutoka kwa Muhammad bin Al-Hasan[17] kutoka kwa Abuw Yuwsuf,[18] na akaisahihisha Ibn Hibbaan, na akaitia kasoro Al-Bayhaqiyy]

 

 

 

817.

وَعَنْ أَبِي قِلَابَةَ، عَنْ أَنَسٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {أَفْرَضُكُمْ زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ سِوَى أَبِي دَاوُدَ، وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ، وَأُعِلَّ بِالْإِرْسَالِ

Kutoka kwa Abuu Qilaabah[19] kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mjuzi wenu katika Faraaidhw (Mirathi) ni Zayd bin Thaabit.”[20] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa Abuu Daawuwd, na akaisahihisha At-Tirmidhiy, Ibn Hibbaan na Al-Haakim, na imepewa dosari kuwa ni Mursal]

 

[1] Faraaidhw ni wingi wa Fardhw yenye maana ya Shariy’ah inayohusu ugawaji wa mirathi.

 

[2] Hawa ni watu wenye mafungu kama walivyotajwa katika Qur-aan nao wanaitwa Dhul-Faraaidhw na warithi wengine wanaowezekana kurithi huitwa ‘Aswabah. Baadhi ya Dhul-Faraaidhw ni ‘Aswabah vile vile. Katika Qur-aan aina sita za mafungu zimetajwa. Hizi ni: Nusu, moja ya nne (robo), moja ya nane (thumuni), theluthi mbili, theluthi moja na sudusi.

 

[3] Hii ikiwa miongoni mwa waliokufa kuna jamaa wasiokuwa Waislamu hawawezi kumrithi. Yaani Muislamu hawezi kumrithi kafiri kama ilivyo kafiri hawezi kumrithi Muislamu.

 

[4] Nusu kwa binti na sudusi kwa mjukuu wa kike (upande wa baba) na theluthi itakuenda kwa dada. Hii ina maana ya kuwa dada akiwa pamoja na binti na mjukuu wanakuwa ni ‘Aswabah

 

[5] Maiti aliacha binti wawili na babu yao kama warithi. Binti wawili watapata theluthi mbili, wakati babu atapata sudusi kama Dhul-Faraaidhw na mwingine sudusi kama ‘Aswabah. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimjulisha kuhusu sudusi ya mwanzo hapo kabla, ili asifikiri fungu lake kuwa ni theluthi kisha akamuelezea mwishoni.

 

[6] Mas-ala haya yako hivi. Maiti aliacha mabinti wawili na babu ambaye ndiye muulizaji, wale mabinti wawili wakapata thuluthi mbili, ikabaki thuluthi moja, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akampa yule muulizaji (Babu) sudus akamuambia “utapata sudusi nyingine ikiwa ni ziada (‘Aswabah).” Kwa hivyo babu amepata sudusi ikiwa ni fungu lake na amepata kilichobakia ikiwa ni ‘Aswabah. Tazama: anayerithi kwa ta’siyb (salio) ni mrithi asiye na kiwango maalumu kilichowekwa na Qur-aan na Hadiyth. Lakini endapo atakuwa yuko peke yake, mali yote itakuwa ni yake, na iwapo atapata fungu na kikabakia kitu hicho kitakuwa ni chake.

 

[7] Al-Hassan bin Abdil-Hassan Al-Baswriyy alikuwa ni mtumwa wa Kianswaar. Babake akiitwa Yassaar. Al-Hassan alikuwa ni Imaam muadilifu. Alikuwa ni madhubuti, mwenye taqwa, Mwanazuoni maarufu, fasaha na mwenye umbuji. Alikua kiongozi wa kizazi cha tatu cha Taabi’iyna, alizaliwa miaka miwili kabla ya ukhalifa wa ‘Umar bin Al-Khatwaab (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuisha. Alipata kumuona ‘Uthmaan bin ‘Affaan na ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) lakini hakupata kupokea Hadiyth kutoka kwao. Alifariki mwezi wa Rajab mwaka 110 Hijriyyah alipokuwa ana miaka 90 takriban.

 

[8] Bibi kwa lugha ya kiarabu ni Jaddah Swahiyhah (mama mzaa baba) na Jaddah Fasiydad (mama mzaa mama). Ikiwa mama wa aliyekufa hayupo, fungu la mama litakuenda kwa mama mzaa baba au mama mzaa mama. Ikiwa wote wapo watagawana fungu hilo.

 

[9] Lau mama atakuwa pamoja naye angalimzuia nyanya kurithi kishariy’ah.

 

[10] Hadiyth hizi ni dalili kuwa ikiwa hakuna ‘Aswabah au Dhul-Faraaidhw (wenye undugu na maiti), kwa hali hiyo basi mjomba anakuwa mrithi. Hii ina maana kwamba mjomba ni mrithi wa mwisho. Ikiwa naye mjomba huyo hayupo mali hiyo itakuenda kwenye Baytul-Maal. Mama mdogo ana nafasi kama nafasi aliyokuwa nayo mjomba.

 

[11] Jina lake ni As’ad au Sa’d lakini alikuwa akijulikana zaidi kama Abuu Umaamah bin Sahl bin Hunayf bin Wahiyb Al-Answaar Al-Aws Al-Madaniy. Alikuwa ni Swahaba na alimuona Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) lakini hakupata kusikia Hadiyth yoyote kutoka kwake. Alifariki mwaka 100 Hijriyyah akiwa na umri wa miaka 92.

 

[12] Huyu ni Abuu ‘Ubaydah ‘Aamir bin ‘Abdillaah bin Al-Jarraah bin Hilaal Al-Qurayshi Al-Fihri. Alikuwa ni mmoja katika kumi waliobashiriwa Jannah. Alisilimu mapema na alihamia Uhabeshi katika Hijrah ya pili. Alishiriki vita vya Badr na vita vinginevyo muhimu pia. Siku ya Uhud alipoteza meno yake mawili alipojaribu kutoa pete ya kofia ya chuma ilipoingia katika kidevu cha Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Abuu ‘Ubaydah aliliongoza jeshi la Kiislam wakati wa kuiteka Shaam. Alifariki katika ugonjwa wa ndui huko Amwaas katika mwaka wa 18 Hijriyyah akiwa na miaka 58.

 

[13] Hii ina maana mtoto yu hai, mtoto huyu anatakiwa kufanyiwa haki zote kama vile kuswaliwa Swalaah ya maiti kama atakufa baada ya hapo na atakuwa na haki ya kurithi na kurithiwa hali kadhalika.

 

[14] Muuaji hana haki ya kurithi katika mali ya aliyeuliwa. Muuaji hapati fungu lolote hata kama akiwa ni ‘Aswabah au Dhul-Faraaidhw wa aliyeuwawa. Aliyeuwa kwa kukusudia na hata kwa kutokusudia wote wako sawa katika hili kulingana na Maimaam wengi isipokuwa Imaam Maalik peke yake.

 

[15] Walaa (Mirathi ya mtumwa aliyeachwa huru) haigawanywi kama mirathi ya Dhul-Faraaidhw. Badili yake, wale ‘Aswabah walio karibu wana haki ya mirathi hiyo (Walaa). Hii ndiyo rai sahihi zaidi ingawaje kuna Wanazuoni wenye rai tofauti.

 

[16] Baada ya kifo cha mtumwa aliyeachwa huru, alichokiacha huitwa Walaa na mwenye kulipa fidia ya uhuru wake huwa ndie mrithi wake baada ya kifo chake aliyekuwa mtumwa ikiwa hana ndugu wa damu wa kumrithi.

 

[17] Huyu ni Abuu ‘Abdullaah Muhammad bin Al-Hassan bin Farqad, Ash-Shaybaan kwa ukoo, alikuwa mmoja wa Maimaam wa dhehebu la Hanafi. Alizaliwa mwaka 132 Hijriyyah huko Waasit na kukulia katika mji wa Kufa huko ‘Iraaq. Alisafiri ili atafute elimu ya Hadiyth na alikutana na Wanazuoni maarufu. Alihudhuria darasa la Abuu Haniyfah kwa miaka, kisha akajifunza elimu ya Fiqhi kwa Abuu Yuwsuf. Aliandika vitabu vingi muhimu na hivyo kutawanya elimu ya Imaam Haniyfah kwa watu wengi. Kadhalika alipata kusoma kwa Imaam Maalik kwa muda wa miaka mitatu. Wanazuoni wa Hadiyth wanaziona Hadiyth alizopokea kama ni dhaifu kutokana na udhaifu wa kumbukumbu yake ilivyokuwa. Alifariki mwaka 189 Hijriyyah huko Ranbuwaih, kijiji kilichopo Ar-Ray.

 

[18] Abuw Yuwsuf alikuwa Mwanazuoni wa Fiqhi huko ‘Iraaq. Jina lake kamili ni Imaam Al-Qaadhw Abuw Yuwsuf Ya’quwb bin Ibrahiym Al-Answaar Al-Kufi, alikua ni mfuasi wa Abuu Haniyfah. Alikulia huku akitafuta elimu. Baba yake alikuwa maskini na Abuu Haniyfah alikuwa akimsaidia baba yake mara kwa mara. Yahya bin Ma’iyn anasema: “Hakuna Mwanazuoni wa Fiqhi ambaye anafahamu Hadiyth au alikuwa madhubuti (katika upokezi wa Hadiyth) kuliko Abuw Yuwsuf.” Yahya bin Yahya At-Tamimi anasema: “Nilimsikia Abuw Yuwsuf akisema wakati wa kifo chake, najikosha na rai ya Fiqhi yoyote niliyoitoa wakati wa uhai wangu isipokuwa inayothibitishwa na Qur-aan na Sunnah katika Riwaayah nyingine isipokuwa ile iliyothibitishwa na Qur-aan na makubaliano ya Waislamu.” Alifariki mwezi wa Rabiy’ Al-Aakhir mwaka 182 akiwa na umri wa miaka 69.

 

[19] Abuu Qilaabah jina lake sahihi ni Zayd bin ‘Amr au ‘Aamir Al-Jurmi Al-Basri. Alikuwa ni Taabi’ maarufu, ni madhubuti na mpokezi wa Hadiyth nyingi zilizokuwa Mursal. Alikuwa katika kizazi cha sita na alifariki Shaam mwaka 104 Hijriyyah au 106 au 107 kwa kukimbia asije akapewa jukumu la Ukadhi.

 

[20] Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwaminifu wa Ummah huu ni Abuu Bakr; mkali zaidi wa Dini ni ‘Umar bin Al-Khatwaab; mpole zaidi miongoni mwao ni ‘Uthmaan; hakimu mzuri zaidi ni ‘Aliy msomaji mzuri wa Qur-aan ni ‘Ubay bin Ka’b; mwenye kujua halaal na haraam miongoni mwao ni Mu’aadh bin Jabal; mjuzi wao wa Faraaidhw ni Zayd bin Thaabit. Jueni kwamba, katika kila Ummah kuna amini wake na amini wa Ummah huu ni Abuu ‘Ubaydah bin Jaraah.” Katika Hadiyth hii Zayd bin Thaabit anatangulizwa kuhusu mas-ala ya migogoro katika mirathi.

 

Share