19-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Biashara: Mlango Wa Al-Luqatwah (Kiokotwa)

 

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَابُ اَلْبُيُوعِ

Kitabu Cha Biashara

 

بَابُ اَللُّقَطَةِ

19-Mlango Wa Al-Luqatwah (Kiokotwa)[1]

 

 

 

 

 

799.

عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {مَرَّ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  بِتَمْرَةٍ فِي اَلطَّرِيقِ، فَقَالَ: " لَوْلَا أَنِّي أَخَافُ أَنْ تَكُونَ مِنَ الصَّدَقَةِ لَأَكَلْتُهَا"} مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Anas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipita akaona tende akasema: Lau kama mimi sichelei tende hii kuwa ni swadaqah ningeila.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

800.

وَعَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ اَلْجُهَنِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: {جَاءَ رَجُلٌ إِلَى اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  فَسَأَلَهُ عَنِ اللُّقَطَةِ ؟ فَقَالَ: " اِعْرِفْ عِفَاصَهَا وَوِكَاءَهَا، ثُمَّ عَرِّفْهَا سَنَةً، فَإِنْ جَاءَ صَاحِبُهَا وَإِلَّا فَشَأْنُكَ بِهَا"

قَالَ: فَضَالَّةُ اَلْغَنَمِ  ؟

قَالَ: "هِيَ لَكَ ، أَوْ لِأَخِيكَ ، أَوْ لِلذِّئْبِ " .

قَالَ: فَضَالَّةُ اَلْإِبِلِ؟

قَالَ: " مَا لَكَ وَلَهَا؟ مَعَهَا سِقَاؤُهَا وَحِذَاؤُهَا، تَرِدُ اَلْمَاءَ، وَتَأْكُلُ اَلشَّجَرَ، حَتَّى يَلْقَاهَا رَبُّهَا} مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Kutoka kwa Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy[2] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Mtu mmoja alikuja kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuuliza kuhusu kilichookotwa. Akasema: Kijue chombo chake na uzi wake kisha kitangaze mwaka mzima. Atapokuja mwenyewe utampa, na asipokuja utaangalia wewe. Na akamuuliza kuhusu mbuzi aliyepotea. Akasema: (Mchukue) ni wako au ni wa nduguyo au ni wa mbwa mwitu. Akamuuliza kuhusu ngamia aliyepotea. Akasema: Unataka kuwafanyia nini? Wana matumbo yao na miguu yao. Wanaweza kuenda kwenye maji na kula majani ya miti hadi wakutane na bwana wao.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

801.

وَعَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {مَنْ آوَى ضَالَّةً فَهُوَ ضَالٌّ ، مَا لَمْ يُعَرِّفْهَا} رَوَاهُ مُسْلِم

Kutoka kwa Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayezuia mnyama aliyemuokota, mtu huyo amepotea maadamu hajamtolea taarifa.”[3] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

802.

وَعَنْ عِيَاضِ بْنِ حِمَارٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ  قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  {مَنْ وَجَدَ لُقَطَةً فَلْيُشْهِدْ ذَوَيْ عَدْلٍ، وَلْيَحْفَظْ عِفَاصَهَا وَوِكَاءَهَا، ثُمَّ لَا يَكْتُمْ، وَلَا يُغَيِّبْ، فَإِنْ جَاءَ رَبُّهَا فَهُوَ أَحَقُّ بِهَا، وَإِلَّا فَهُوَ مَالُ اَللَّهِ يُؤْتِيهِ مَنْ يَشَاءُ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ، وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَةَ، وَابْنُ اَلْجَارُودِ، وَابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa ‘Iyaadhw bin Himaar[4] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Anayepata kitu alichookota ashuhudishe waadilifu wawili[5] na ahifadhi chombo chake na uzi wake kisha asikifiche wala asikifunike, mwenyewe akija basi ana haki (na kitu chake) na asipokuja hiyo ni mali ya Allaah Humpa Amtakaye.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Ibn Khuzaymah, Ibn Al-Jaaruwd na Ibn Hibbaan]

 

 

 

803.

وَعَنْ عَبْدِ اَلرَّحْمَنِ بْنِ عُثْمَانَ التَّيْمِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ  نَهَى عَنْ لُقَطَةِ اَلْحَاجِّ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Uthmaan At-Taymiyy[6] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amekataza mtu kuokota alichopoteza Haajj (mwenye kuhiji).”[7] [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

804.

وَعَنْ اَلْمِقْدَامِ بْنِ مَعْدِ يكَرِبَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {أَلَا لَا يَحِلُّ ذُو نَابٍ مِنَ السِّبَاعِ، وَلَا اَلْحِمَارُ اَلْأَهْلِيُّ، وَلَا اَللُّقَطَةُ مِنْ مَالِ مُعَاهَدٍ، إِلَّا أَنْ يَسْتَغْنِيَ عَنْهَا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ

Kutoka kwa Al-Miqdaam bin Ma’d Yakrib[8] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Fahamuni! Si halaal kula wanyama mwitu, wala kula punda wa mjini, wala kuokota kutoka katika mali ya dhimmi[9] isipokuwa kiwe ni kitu kisichohitajika.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]

 

[1] Al-Luqatwah ni kitu kilichoanguka au kupotea. Shariy’ah imegawanya katika mafungu matatu: i-kama ni kitu duni au chakula kinaweza kuokotwa na kuliwa. ii-Kitu cha kawaida kisicholiwa; kinaweza kuokotwa na mtu atangaze hadharani siku tatu. iii-Kitu chenye thamani ambacho shariy’ah inaamrisha; Kikiokotwa kitangazwe muda wa mwaka. Kisha ikiwa mweyewe atapatikana arudishiwe. Laa sivyo kinaweza kutumiwa. Kuna rai za kukhitilafiana kuhusu nukta hii kama kurudishiwa mwenyewe  au laa ikiwa atapatikana mwenyewe baada ya kuwa kimeshatumiwa.

 

[2] Lakabu yake ni ni Abuu ‘Abdir-Rahmaan au Abuu Twalhah Zayd bin Khaalid Al-Juhaniyy Al-Madaniy, ni mkazi wa Madiynah. Swahaba maarufu. Alikuwa amebeba bendera ya watu wa kabila la Juhaynah katika siku ya Fat-h Makkah (Ufunguzi wa Makkah). Aliishi katika mji wa Kufa. Alifariki Madiynah mwaka wa 78 Hijriyyah akiwa na umri wa miaka 85.

 

[3] Ikiwa mtu ataokota kitu kilichopotea au kumuanguka mtu na akawa na niyyah ya kukitangaza, au kuwazuiwa watu anaodhania wakichukua hawatotangaza inafaa kufanya hivyo. Kuchukua au kuokota kitu kwa niyyah mbaya ya kukihodhi haitakiwi na ni jambo ambalo halipendezi kishariy’ah.

 

[4] ‘Iyaadhw bin Himaar At-Tamiym Al-Mujashi’ ni Swahaba aliishi Basra (‘Iraaq) hadi miaka ya 50 Hijriyyah

 

[5] Ikiwa kilichookotwa chenyewe ni kitu kilichopotea au kilichodondoka, wanahitajika mashahidi wawili mara moja. Vile vile, wakati wa mwenyewe kuja kukichukua mashahidi waitwe vile vile kushuhudia. Mashahidi wote hao ni muhimu sana. Hii ni kwa sababu mwenye nacho akishachukua anaweza kujitokeza mtu mwingine ambaye atatoa wasifu ule ule wa kiokotwa na kudai kuwa ni chake na hili litapelekea kwenye mzozo.

 

[6] ‘Abdur-Rahmaan bin ‘Uthmaan At-Taymiyy Al-Qurayshi, ni mpwa wa Twalhah bin ‘Ubaydillaah, ni Swahaba. Inasemekana kuwa pamoja ya kuwa aliishi katika zama za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) lakini hakuwahi kukutana naye. Alisilimu wakati wa Hudaybiyah au katika Fat-h ya Makka. Aliuawa pamoja na ‘Abdullaah bin Az-Zubayr katika mwaka 73 Hijriyyah.

 

[7] Hii ni kwa sababu Haajj ni msafiri na ni nadra kwa Haaj kukutana na aliyeokota kiokotwa, ndiyo maana ikawekwa amri ya kutookota alichokipoteza au alichokiangusha Haajj. Na hii ni zaidi kwa mwenye niyyah ya kukimiliki.

 

[8] Al-Miqdaam bin Ma’d Yakrib bin ‘Amr Al-Kindiy, aliyejulikana kwa Abuu Karimah au Abuu Yahya. Alikuwa ni Swahaba maarufu. Aliishi Shaam na Hadiyth yake ilienea kwa watu wengi sana katika watu wake. Alifariki mwaka 47 Hijriyyah akiwa na umri wa miaka 91.

 

[9] Dhimmi ni kafiri anayeishi katika Dola ya Kiislamu na anayefuata shariy’ah za nchi na Mu’ahid mtu kafiri anayetembelea nchi za Kiislamu akiwa na ruhusa ya kusafiri visa na akifanya shughuli zake kwa amani. Dola ya Kiislamu ni jukumu lake kuangalia amani yake na mali zake n.k. Hakuna tofauti kati ya kiokotwa cha dhimmi, Mu’ahid na Muislamu kadiri ya shariy’ah ya kiokotwa inavyohusika. Hata hivyo kikiwa ni kitu duni kinaweza kuokotwa.

 

Share