Imaam Ibn Taymiyyah: Zawadi Hazifai Kupokelewa Wala Kutoa Katika Sherehe Zisizokuwa Za Kiislamu
Zawadi Hazifai Kupokelewa Wala Kutoa Katika Sherehe Zisizokuwa Za Kiislamu
Imaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah)
“Yeyote atakayempa Muislamuu zawadi katika sherehe hizi, siku ambazo si siku za kawaida basi zawadi hiyo haikubaliki, hususan ikiwa zawadi hiyo inapelekea katika kushabihiana nao, mfano mshumaa na kadhalika kama vile siku za kuzaliwa au mayai, maziwa, kondoo siku ya Alkhamiys ambayo huwa ni mwisho wa kufunga swiyaam zao. Vile vile, Musilamu hawapasi kutoa zawaida katika sherehe zao hizo hususan ikiwa itapelekea katika kufanana nao kama tulivyotaja.”
[Iqtidhwaa As-Swiraatw Al-Mustaqiym(1/227)]