04-Zawadi Kwa Wanandoa: Kutanguliza Na Kuchelewesha Mahari
Zawadi Kwa Wanandoa
04-Kutanguliza Na Kuchelewesha Mahari
المعجّل والمؤجّل
Inafaa na inajuzu kutanguliza na kuchelewesha mahari. Kulipa mwanzo na nyingine kuchelewa kama ilivyo kuwa ni ada na desturi ya mahala na uwezo wa mtu.
Lakini kinachofaa zaidi ni kutanguliza chochote kwa yaliyopokewa na ibn Abbas kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) alimkataza Ali kumuingilia bibi Fatma mtoto wake hadi awe ametoa chochote katika mahari. Ali (Radhiya Allaahu 'anhu) akasema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) , ‘Sina chochote’. Akasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) : ‘Liko wapi deraya lako la kihutwamiyya?’ Akampa ikawa ndio mahari yake.” (Abu Daawuwd, An-Nasaaiy na Ahmad)
Na akasema bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) : “Ameniamrisha mimi Mtume (Swalla Llaahu 'alayhi wa sallam) nimuingize mwanamke kwa mumewe kabla hajampa chochote.” (Abu Daawuwd).