05-Zawadi Kwa Wanandoa: Chombo

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

05-Chombo  

 

الجهاز

 

 

 

 

 الجهاز   ni kutayarisha anachokihitaji bibi harusi katika vyombo vya nyumbani kama vile fanicha ili aweke nyumbani kwake. Kilichozoeleka ni kuwa Bibi harusi na ndugu za bibi harusi ndio wenye kutayarisha vyombo hivyo na kuvipanga na kuitengeza nyumba, na wengineo huwa wana tabia ya kuvionyesha vyombo hivyo kwa sherehe na hafla za wazi. Leo hii sherehe kama hizi zinaishia katika mitaa wanayoishi watu wa hali ya chini, ‘Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  alimtayarishia vyombo bibi Faatwimah ndani yake pana nguo zilizofumwa kwa manyoya ya mbuni, na kiriba cha kuwekea maji na mto wa kulalia uliowekewa mmea wenye harufu nzuri.’ (An-Nasaaiy).

 

 

 

Share