10-Zawadi Kwa Wanandoa: Usia wa Mama kwa Bintiye

 

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

10- Usia wa Mama kwa Bintiye

 

وصيّة الأم لا بنت

 

 

 

Amru bin Hujri aliposa kwa Malik kan-da, kumposa Ummu Iyaas binti Auf bin Muhalim Asshaybaniy, na ilipofika siku ya sherehe ya ndoa yake Mama yake Umama bint al-Harith alichepuka nae pembeni na kumuusia,

 

"Ee, Binti yangu: hakika usia ukiachwa kwa fadhila ya adabu (yaani isingekuwa na haja ya kuwausia wenye adabu nzuri) ningeliacha kwako, lakini usia mwanangu ni ukumbusho kwa msahaulifu, na msaada kwa mwenye akili. Na lau kwamba mwanamke asingemuhitajia mume basi wazazi kadhalika wasingehitajika. Ni muhimu sana haja zao kuwa pamoja, basi mimi ningekuwa ni mtu nisiyemhitajia baba yako, lakini mwanangu wanawake kwa wanaume wameumbiwa, na wao wameumbwa kwa ajili ya wanaume.

Ee, Binti yangu: Hakika wewe unaacha mazingira uliyoyazoea na unaacha maisha uliyokulia, unakwenda usipopajua na mwenza usiyemzoea, na atakuwa ndie mwangalizi wako, hivyo basi kuwa kwake kijakazi nae atakuwa ni mtumwa wako asiyetamani kukukosa. Hifadhi kwake mambo kumi, atakuwa kwako hazina:

 

1) Unyenyekee kwake kwa kukinai.

 

2) Umsikilize vizuri na kumtii.

 

3) Na uangalie maeneo ya macho yake na pua yake.

 

4) Hivyo basi, macho yake yasione au kuangalia yanayochukiza kwako na wala yasinuse ila harufu nzuri kutoka kwako.

 

5) Angalia wakati wake wa kulala na chakula chake.

 

 6) Kwani hakika mbabaiko wa njaa unaunguza na kukosa usingizi kunaghadhibisha.

 

 7) Chunga mali yake na ulinde heshima yake na watoto wake.

 

 8) Na matumizi ya mali yawe mazuri na katika kuishi nae upange vizuri maisha.

 

9) Usimuasi kwa jambo na usitoe siri zake.

 

10) Kwani wewe ukikengeuka na amri yake utapandisha chuki na hasira katika kifua chake, na ukitoa siri zake hutosalimika kwa kumvunjia ahadi yake, kisha ole wako na kufurahi hali yakuwa hana raha, na kukasirika hali ya kuwa amefurahi."

 

 

Share