09-Zawadi Kwa Wanandoa: Wasia wa Mume kwa Mkewe
Zawadi Kwa Wanandoa
09- Wasia wa Mume kwa Mkewe
وصية الزّ وج إلى زوجته
Amesema Abu Dardaai kumuusia mkewe: ‘Ukiniona mimi nimekasirika jaribu kuniridhisha, nami nikikuona umekasirika nitakuridhisha, vinginevyo hatutoweza kukaa pamoja.’
Na akasema mmoja wa waume kumwambia mke wake:
Chukua msamaha wangu yatadumu mapenzi yangu (mawadda),
Wala usizungumze katika kilele cha ghadhabu
pindi ninapo ghadhibika.
Wala usinigonge kwa mgongo wako hata mara moja
Kwani wewe hujui ni wapi jua linapozamia
Na wala usizidishe malalamiko na nguvu kuondoka
Na moyo wangu ukakukataa, na mioyo hugeuka
Nami nimeona mapenzi katika moyo na maudhi vile vile
Zikikutana, basi mapenzi hayakai yataondoka.”