08-Zawadi Kwa Wanandoa: Wasia wa Baba kwa Mkwe Wake

 

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

08-Wasia wa Baba kwa Mkwe Wake

 

وصيّة العم لصهره

 

 

 

'Aliy bin Abi Tawalib (Radhiya Allaahu 'anhu)  alipo posa kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kumposa mtoto wake Fatma, alisema Mtume juu yake sala na salamu:

 

"هي لك على أن تحسن صحبته"

 

“Huyo ni wako maadamu utaufanyia uzuri usuhuba wake.” (Imepokewa na Abu Na'iym)

 

 

 

Na 'Uthmaan bin Anbasa bin Abi Sufyaan akaposa kwa 'Ami yake 'Utbah kutaka kumuoa binti yake, akamkalisha ubavuni mwake na akaanza kupangusa kichwa chake, kisha akamwambia,  ‘Mtu wa karibu zaidi (ndugu) amemposa ninayempenda zaidi, siwezi kumrudisha, na sina sababu ya hilo. Nimekuozesha nawe ni azizi kwangu zaidi kuliko binti yangu, naye moyo wake umegandana nami zaidi kuliko wako, hivyo mkirimu na ulimi wangu utaona tamu kukutaja, wala usimshushie hadhi yake ikapungua hadhi yako kwangu, na nimekuweka karibu pamoja na ukaribu wa udugu tulionao, hivyo basi usiupeleke moyo wangu mbali na moyo wako.’

 

 

 

 

 

 

Share