07-Zawadi Kwa Wanandoa: Wasia Wa Baba Kwa Binti Yake
Zawadi Kwa Wanandoa
07- Wasia Wa Baba Kwa Binti Yake
وصيّة الأب ابنته
'Abdullaah bin Ja'far bin Abi Twaalib amemuusia binti yake kwa kumuambia, ‘Ole wako na wivu, nao ni ufunguo wa Talaka. Na ole wako na malalamiko mengi, nayo hupelekea katika bughudha. Na jitie wanja kwani huko ndiko kujipamba kuzuri zaidi. Na kizuri katika vizuri zaidi ni Maji.’