16-Zawadi Kwa Wanandoa: Swalah Ya Sunnah Kwa Wanandoa

 

Zawadi Kwa Wanandoa 

 

16-Swalah Ya Sunnah Kwa Wanandoa

 

سنّة صلاة الزّواج

 

 

 

Usiku wa mwanzo wa Mume na Mke si kwa ajili tu ya kujifurahisha pekee na raha ya kuingiliana bali ni lazima kutekeleza amri za Dini na katika hayo ni Swalah. Amesema Mtume (Swalla Allaah 'alayhi wa sallam) :

 

إذا تزوّج أحدكم فكانت ليلة البناء فليصلّ ركعتين , وليأمرها أن تصليّ خلفه , فإنّ الله جاعل في البيت خيرا

 

“Atakapooa mmoja wenu na ikawa ni siku ya mjengo na aswali rakaa mbili na amuamuru mke wake aswali nyuma yake, kwani Allaah Atajaalia katika nyumba hiyo kheri.”

(Imepokewa na al-Bazaar kama ilivyo katika kashfu al-Astaar)

 

Mtume Amesema juu yake Swalah na amani:

 

إذا دخلت المرأة على زوجها يقوم الرّجل فتقوم من خلفه فيصلّيان ركعتين ويقول : اللهم بارك لي في أهلي وبارك لأهلي فيّ , اللهم ارزقهم مني , وارزقني منهم , اللهم اجمع بيننا ما جمعت في خير , وفرّق بيننا إذا فرّقت إلى خير

 

“Atakapoingia mwanamke kwa mumewe, atasimama mwanamme na mwanamke atasimama nyuma yake, na wataswali rakaa mbili na atasema: Ee Allaah! Nibarikie mimi kwa ahli zangu na uwabariki kwangu ahli zangu, ee Allah! Waruzuku wao kwangu na uniruzuku mimi kwao, ee Allaah! Tuunganishe mimi na mke wangu katika muunganisho wa kheri, na Utufarikishe

baina yetu kwa kheri pindi Utakapotufarikisha.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Share