22-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuharamisha Kuingilia Katika Tupu Ya Nyuma
Zawadi Kwa Wanandoa
22-Kuharamisha Kuingilia Katika Tupu ya Nyuma
تحريم نكاح الدّبر
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
نساؤكم حرث لكم فأتوا حرثكم أنى شئتم
“ Wake zenu ni konde zenu, basi ziendeeni konde zenu mpendavyo.” (Al-Baqarah: 223)
Ilikuwa ni tabia ya Mayahudi wakisema: Mtu atakapomuingilia mke wake mbele lakini kwa upande wa nyuma basi atazaliwa mtoto akiwa ni kengeza; ikashuka Aayah hii:“Wake zenu ni mashamba yenu.” (Muslim). Katika riwaya nyingine:
إن شاء مجبّية و إن شاء غير مجبّية غير أنّ ذلك في صمام واحد
“…na ukipenda ufanye staili ya kama anasujudu na ukipenda sivyo hivyo yote ni sawa sawa...” (Muslim: Hadithi 1435)
Ilikuwa ni tabia ya Ahlul-Kitaab kutomuingilia mwanamke ila kiubavu na katika hali ya mwanamke kujistiri. Na ilikuwa tabia ya baadhi ya Answaar kuiga tabia zao hizo. Na wanaume wa ki-Quraysh walikuwa wamezowea kufanya mapenzi na wake zao vilivyo, wakistarehe nao kwa mbele, nyuma na kwa chali, (lakini bila ya kuwaingilia tupu zao za nyuma). Walipohamia Muhajirina Madiynah alioa mmoja wao mwanamke wa ki-Answaar; akataka kufanya nae mapenzi kwa mitindo waliyozoea (huko Makkah) akachukizwa mwanamke yule na hilo, na akasema: Hakika sisi tulikuwa tukiingiliwa kiubavu, fanya hivyo au niepuke; kisa chao kikaenea, zikamfikia habari Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na Allaah Akashusha:
نساؤكم حرث لكم
“Wake zenu ni konde zenu…” (Abu Daawuwd)
Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema vile vile:
“(Waingilieni wake zenu kwa mtindo wa) Kwa mbele au (kwa mtindo wa) kwa nyuma lakini epukeni dubur (utupu wa nyuma) na (kuwaingilia wakati wako) kwenye hedhi.”(At-Tirmidhiy)