23-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuoga Katika Chombo Kimoja
Zawadi Kwa Wanandoa
23-Kuoga Katika Chombo Kimoja
الإغتسال من إناء واح
Inajuzu kwa wanandoa wawili kuoga pamoja katika sehemu moja, imepokewa kutoka kwa 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha) amesema:
“Nilikuwa nikioga mimi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) katika chombo kimoja, inapishana mikono yetu ndani yake, na ananianza kwa hilo hadi nasema: niachie … niachie. Akaendelea kusema Bibi 'Aaishah wakiwa hivyo hali ya kuwa ni wenye janaba.” (Muslim)