24-Zawadi Kwa Wanandoa: Kuondosha Bikira
Zawadi Kwa Wanandoa
24-Kuondosha Bikira
فض غشاء البكارة
Utando wa bikira unatofautiana kutoka kwa mwanamke mmoja hadi mwingine, baadhi yao bikira zao ni khafifu hukatika na kuachia mara moja kwa kuanguka, na baadhi nyingine ni ngumu. Hivyo basi anatahadharishwa mume katika kufahamu na kujua kuwa ule utando wa bikira wenyewe ndio kipimo cha usafi na utukufu wa mwanamke. Katika ada zilizo mbovu kabisa ni ile hali ya baadhi ya wanaume kuondosha bikira kwa kutumia vidole vyao, na haya ni madhara makubwa kwa mwanamke na humsababishia maudhi mengi.
Jambo jingine ambalo ni baya ni zile hila za kisheitani wanazotumia baadhi ya wasichana wasiojitunza na ambao wanawahadaa waume zao siku ya mwanzo ya harusi kwa hila zenye kufahamika na madaktari na makungwi.
Jukumu kubwa linaloonekana kwa waume wengi ni kuondosha utando wa bikira siku ile ile ya mwanzo kwa njia yoyote na husubiri mke wake ajisalimishe kwake kwa hilo. Na wakati mwingine msichana al-huyiyya (bado hajamuona mwanamme) anaweza kukataa na baadhi ya wasichana hufikiri kuwa ndoa ni mchezo na matembezi hivyo basi akimuona mwanamme amevua nguo zake na uume wake umesimama akiwa ni mwenye pupa na jambo lake huanza kuogopa na huenda akaupiga ukelele na hujaribu kujizuia na mume wake na hii inarejea na uduni wa uzoefu wa wote wawili mume na mke na kuwa na fikra mbovu kuhusu ngono.