25-Zawadi Kwa Wanandoa: Kumchezea Mke
Zawadi Kwa Wanandoa
25-Kumchezea Mke
مداعبة الزّوجة
Hakika katika jambo ambalo ni muhimu kwa mume kulichunga na kulilinda ni kumchezea chezea mke wake na haswa kabla ya kumuingilia, hili lina athari kubwa sana kati ya wanandoa wawili katika mahusiano yao ya kiroho na ya kijinsi.
Katika kufikia kilele cha raha ya kiwiliwili kunahitaji kwa mwanamme awe na diplomasia ili aweze kumpa mke wake hamu na matamanio ya kweli, na ushiriki mzuri ulio kamili na mapenzi yaliyokita.
Mke mwenye hekima anaweza kwa diplomasia aliyokuwa nayo na mapambo yake na usafi wa kiwiliwili chake kumvuta mume wake na kumtamanisha. Hivyo basi kumhimiza katika kuwasiliana kwa kiwiliwili vyao kwa urahisi na wepesi zaidi, mahaba siku zote yanatimiza furaha.
Ama kumuingilia mwanamke bila ya kuwepo vitangulizi huwa ni jambo lisilofaa na la kinyama la kutosheleza mahitaji ya mwanamme, kisha haupiti muda mrefu kamaliza haja na kukaa mbali ya mwanamke hali ya kuhema!.
Mwanamke siku zote hupendelea mumewe ashirikiane nae katika hisia zake kwa upole na wema na acheze nae kwa muda unaotosha kupandisha hamu na nyege zake. Na hivi vitangulizi vya jimai husaidia kuwafikisha wanandoa wawili katika utulivu kamili na hivyo kufikia kilele cha raha ya tendo la ndoa.
Kwa hilo na mengineyo Uislamu unahimiza suala hili la kuchezeana na kumchezea mke, amesema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :
كلّ شيئ ليس من ذكر الله , لهو ولعب إلاّ أن يكون أربعة: ملاعبة الرّجل امرأته و تأديب الرّجل فرسه ومشي الرّجل بين الغرضين وتعليم الرّجل السّباح
“Kila kitu katika lahau na mchezo si katika dhikri ya Allah ila iwe ni kimoja katika hivi vinne: 1) Mwanamme kumchezea mke wake. 2) Mtu kumfundisha farasi wake. 3) Na mtu kutembea katika kamba mbili za juu au milingoti miwili. 4) Na mtu kujifunza kuogelea.” (At-Tirmidhiy)
Na katika kuchezeana suala muhimu ni upole na ulaini na kumsubiri mkeo hadi amalize haja yake kwani wakati mwingine huchelewa, ni bora kwa mwanamme ajipambe na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) :
لا يؤمن أحدكم حتى يحبّ لأخيه ما يحبّ لنفسه
“Hatoamini mmoja wenu hadi ampendelee nduguye lile analolipendelea katika nafsi yake.” (Al-Bukhaariy na Muslim)
na ukweli ni kwamba hakuna aliyekuwa karibu kufanyiwa hayo isipokuwa ni mke.
Tukiulizana ni vipi mwanamme anafika kilele cha ladha ya jimai? Utaona kwamba ufumbuzi unapatikana katika hali zifuatazo. Kuamini kuwa tendo la Ndoa ni Ibada: