29-Zawadi Kwa Wanandoa: Kutafuta Raha Bila Ya Jimai

 

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

29-Kutafuta Raha Bila Ya Jimai

 

 الاستمتاع دون جماع

 

 

Je mwanamke akiwa katia udhuru, kwa kuwa ni mwenye hedhi, mwanamme huruhusiwa kumchezea mkewe? Au amtelekeze na kumtenga kabisa kwa sababu hiyo?

 

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  ana msemo maarufu kuhusu wanawake wenye hedhi, anasema:

 

اصنعوا كلّ شيئ إلاّ النّكاح

 

“Fanya kila kitu isipokuwa kumuingilia.”

(Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy na Ibn Maajah)

 

Na imepokewa kwa wake za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  kuwa Mtume“Anapotaka kustarehe na mke wake mwenye hedhi basi hufunika tupu ya mwanamke.”(Abu Daawuwd). Na kutoka kwa Bibi 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anha)  amesema:“Alikuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam)  akimuamuru mmoja wetu akiwa na hedhi ajifunge shuka kwenye tupu yake kisha humchezea.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

 

Mahusiano ya mke na mume hayaishii katika Jimai peke yake bali yanakusanya kuona raha katika uke wa mke na hisia nyingine za kibinaadamu kama vile kunusa, kukumbatia, na kuchezeana, michezo mingine ya kuchekesha na kushikana shikana kwa aina zote mbali na tendo lenyewe la Jimai. Na hii hufanikisha hamu na matamanio ya kubadilishana baina ya wanandoa wawili. Kwa mwanamke mwenye hedhi huku kutomaswatomaswa humsaidia kumpunguzia ule usumbufu aupatao katika hedhi yake na lingine muhimu zaidi ni kufahamu vile vile kuwa yeye si chombo tu cha kushibisha matamanio ya kingono ya mumewe peke yake bali kuna mambo mengine amabayo ni muhimu vile vile mbali na kule kushuka na kumwaga.

 

Share