30-Zawadi Kwa Wanandoa: Uhuru Wa Kuangalia Uchi
Zawadi Kwa Wanandoa
30-Uhuru Wa Kuangalia Uchi
حريّة النّظر إلى العورات
Baadhi ya Majahili hudhani kuwa kuanglia tupu ni haramu au makruhu, na kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) amekataza hilo na kulitahadharisha nalo watu, na wanapokea kwa Aisha kuwa amesema: sikupata kuona uchi wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) hata siku moja. Hadithi hii imebatilishwa na Haafidhw Ibn Hajar, kuwa ni uongo mtupu na imezushwa.
Na ndivyo hivyo imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) kuwa amesema: “Atakapomuingilia mmoja wenu mke wake basi asimuangalie kwenye tupu yake kwani hiyo hupelekea mtu kuwa kipofu.” Na hadithi hii ni Mawdhuw'(imezushwa) kama alivyosema Ibn al-Jawziy na Abu Haatim alrRaaziy.
Na sisi hapa tunasema kuwa amepokea At-Tirmidhiy na Abu Daawuwd na wengineo kutoka kwa Mu'aawiyah bin Hayda amesema: nilisema: Ee, Mtume wa Allaah, uchi wetu, tunaingilia na kuangalia? Akasema:
احفظ عورتك إلاّ من زوجتك أو ما ملك يمينك
“Hifadhi uchi wako ila kwa mke wako au kwa wale unaowamiliki mkono wako wa kuume.”
(Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ahmad)
Na hii ni dalili tosha ya kuruhusu kuangaliana uchi baina ya mke na mume.