38-Zawadi Kwa Wanandoa: Uwastani Katika Wivu

 

Zawadi Kwa Wanandoa

 

38-Uwastani Katika Wivu

 

الاعتدال في الغير

 

 

Huu uwastani unaokusudiwa hapa ni kutoghafilika na mambo ambayo matokeo yake huogopwa siku zote, na kutozidisha dhana na dhulma katika kuhesabu mambo.

 

Amesema mbora wa viumbe juu yake Swalah na amani:

 

إنّ من الغيرة غيرة يبغضها الله عزّ وجلّ وهي من غيرة الرّجل على أهله من غير ريبة

 

“Hakika katika wivu ni wivu unaombughudhi Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)  nao ni wivu wa mwanamme kwa mkewe katika kisichokuwa na shaka.” (An-Nasaa, Ibn Maajah na Ad-Daarimy)

 

Swahaba 'Aliy bin Abi Twaalib (Radhiya AAllaahu 'anhu) anasema:

 

لا تكثر الغيرة على أهلك فترمى بالسوء من أجلك

                                                                                                                                                                                      

“Msizidishe wivu kwa wake zenu ukaangukia  uovu kwako.”

 

Wivu unatakiwa na ni muhimu ili kulinda hadhi ya mtu na ikithibiti sehemu yake basi inapendeza na kupongezwa na shsri'ah, katika hili Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) ana haya ya kusema:

 

 إنّ الله يغار , والمؤمن يغار, وغيرة الله تعالى أن يأتي الرّجل ما حرّم عليه

“Hakika Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Huona wivu na muumini huona wivu na Wivu wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Unakuwa pindi mtu anapofanya alichoharamishiwa.” (Al-Bukhaariy na Muslim)

 

Leo hii watu ambao hudhani kuwa wamestaarabika huchukuwa wake zao wakiwa wamekamilika kwa mapambo yao huenda na kukesha na marafiki zake katika sehemu za starehe na wakati mwingine humtoa kwa aliyemuomba acheze na mke wake na hana wasiwasi kabisa, Je, huku si kufa kwa nafsi za wivu kwa watu hawa?!

 

Suluhisho la amani la tatizo hili ni kutochanganyika wanaume na wanawake. 'Aliy (Radhiya Allaahu 'anhu)  alikuwa siku moja kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) akasema: “Ni kitu gani bora kwa mwanamke? Hawakujibu kitu na niliporejea nilimwambia Fatima: Je, ni kitu gani bora kwa mwanamke? Akasema: “Asifanyiwe rehani mumewe. Nikalitaja hilo kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) .”Akasema: “Huyo (aliyekuambia) ni fatima nae ni sehemu yangu (damu yangu).” (Al-Bazaar)

 

Ibn al-Qayyim amesema: Asili ya Dini ni wivu, na asiyekuwa na wivu hana dini, na wivu unalinda moyo na huo moyo unalinda kiwiliwili, hivyo basi huuzuia moyo kufanya uovu na uchafu. Na kukosekana kwa wivu hufisha moyo hivyo basi na kiwiliwili kizima hufa, hivyo anakosa kinga ya kujizuia na maovu na machafu.

 

Mfano wa wivu ni kama ile nguvu inayozuia maradhi na kuukinga mwili, hivyo kinga hiyo ikiondoka ugonjwa huingia sehemu ile ya mwili na hukosa cha kuizuia na kuilinda, hivyo ugonjwa hukaa, na hapo ndipo penye maangamizi yenyewe.

 

Share