Shaykh Fawzaan: Mitihani Na Majaribio Huzunguka Baina Ya Watu
Mitihani Na Majaribio Huzunguka Baina Ya Watu
Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
Dunia si daima yenye neema na wasaa na starehe na furaha na nusra; haipo daima hivyo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyozungusha baina ya waja.
Maswahaba ni ummah bora kabisa lakini imewafika mitihani mingapi na majaribio?
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ
Na hizo ni siku Tunazizungusha zamu (za mabadiliko ya hali) baina ya watu [An-Nisaa: 140]
Basi mja ajiandae nafsi yake kwamba anapopatwa na mtihani basi (atambue) huo si mahsusi pekee bali imewafika vipenzi wa Allaah. Basi ajiandae nafsi yake na avute subira na angojee faraja kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na mwisho mwema ni kwa wenye taqwa.
[Sharh Al-Qawaaid Al-Arba’]