Imaam Ibn Baaz: Fadhila Za Maiti Kuswaliwa Na Idadi Ya Watu Wengi

 

Fadhila Za Maiti Kuswaliwa Na Idadi Ya Watu Wengi

 

Imaam Ibn Baaz (Rahimahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, inapokuwa idadi ni kubwa ya wanaomswalia maiti kuna fadhila?

 

 

JIBU:

 

Imethibiti katika Hadyth ya Ibn ‘Abbaas kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amesema:

 

((مَا مِنْ رَجُلٍ مُسْلِمٍ يَمُوتُ، فَيَقُومُ عَلَى جَنَازَتِهِ أَرْبَعُونَ رَجُلًا، لَا يُشْرِكُونَ بِاَللَّهِ شَيْئًا، إِلَّا شَفَّعَهُمْ اَللَّهُ فِيهِ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Muislamu yeyote anapofariki na wakasimama watu arubaini wasio mshirikisha Allaah na chochote wakamswalia, Allaah Atawakubali wawe waombezi wake.” [Muslim]

 

Na kwa hivyo, ‘Ulamaa wamependelea kukimbilia Msikiti unaoswaliwa na watu wengi kwa ajili ya kumswalia maiti. Na kila inapokuwa idadi (ya watu) ni kubwa, basi huwa karibu zaidi na khayr na kukithiri du’aa.”

 

 

[Al-Mawqi’ Ar-Rasmiy lil-Imaam Ibn Baaz]

 

 

Share