Shaykh Fawzaan: Maana Ya “Macho Hayamzunguki”

 

Maana Ya “Macho Hayamzunguki”

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu-Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

Shaykh Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) amesema:

 

“Na maana “Bila kuzunguka wala kayfiyah (kuzunguka vipi”, wao hawamzunguki Allaah (‘Azza wa Jalla), na kwamba wao wanamuona (Allaah) Subhaanahu bila ya kumzunguka. Na Allaah Mtukufu haiwezekani Yeye  kuzungukwa.

 

Anasema Subhaanahu:

وَلَا يُحِيطُونَ بِهِ عِلْمًا ﴿١١٠﴾

na wala hawawezi kufikia kuelewa chochote cha ujuzi Wake. [Twaahaa: 110]

 

 

Na Anasema Jalla Wa ‘Alaa:

 

لَّا تُدْرِكُهُ الْأَبْصَارُ وَهُوَ يُدْرِكُ الْأَبْصَارَ  

Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote. [Al-An’aam: 103]

 

“Macho hayamzunguki”

 

Maana yake (katika Aayah hiyo) ni kuwa, “Hayamzunguki Yeye (macho ya mtu)”, na wala maana yake si “Hayamuoni.” Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta’alaa) Hakusema, “Hayamuoni Yeye macho.” bali Kasema, “Macho hayamzunguki.” Kudiriki ni kitu na kuona ni kitu kingine.

 

Hayo (macho) yanamuona Subhaanahu bila kumzunguka (pande zote kwa uoni), na kwa hili kuna radd (majibu ya kukanusha) kwa yule mwenye kustadili (kutolea dalili) kwa Aayah hii kupinga kuonekana Allaah Qiyaamah. Akidai (mpotevu huyo) kuwa haiwezekani kuonekana Allaah, kwa sababu Allaah Kasema, “Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote;” [Al-An’aam: 103]

 

Tunawajibu (wenye itikadi hizo potofu), kuwa nyinyi hamfahamu maana ya “Macho hayamzunguki bali Yeye Anayazunguka macho yote”, bali maana yake ni “Hayamzunguki Yeye macho” na si maana yake “Hayamuoni Yeye”, na Hakusema Allaah, “Hayamuoni Yeye macho.”

 

 

[At-Ta’liyqaat Al-Mukhtaswarah ‘Alaa Al-‘Aqiydati Atw-Twahaawiyyah, mj. 1, uk. 78]

 

 

Share