Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Itikadi Ya Kupindua Viatu Vinapopinduka Haina Dalili
Itikadi Ya Kupindua Viatu Vinapopinduka Haina Dalili
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Baadhi ya watu wanasema kuwa kuweko viatu vilivyopinduka juu chini inamaanisha kwamba Malaika haingii katika nyumba hiyo au Allaah Hatoitazama nyumba hiyyo. Je, mnasemaje kuhusu jambo hili?
JIBU:
Tunasema: Hii hakuna dalili yake wala sijui kama kuna kuhusu kupinduka viatu. Lakini jambo hili limekuwa maarufu kwa watu huenda jambo likawa maarufu kwa watu lakini halina dalili.
(Nuwr Alaa Ad-Darb (13/65)]
