Imaam Ibn 'Uthaymiyn: Kutaja Jina La Allaah Msalani
Kutaja Jina La Allaah Msalani
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah)
SWALI:
Je, inajuzu kumdhukuru Allaah akiwa msalani? Yaani sehemu za kujisaidia haja kama chooni, msalani, bafuni kama vile kusema “Subhaana Allaah” au “AstaghfiruLLaah” anapokuwa amekaa kujisaidia (haja ndogo au kubwa)?
JIBU:
Inalojulikana kwa wengi miongoni mwa ‘Ulamaa ni kwamba inachukuza kutaja kwa ulimi Jina la Allaah (anapokuwa msalani). Ama kumdhukuru moyoni mwake na kuendelea kufanya hivyo moyoni, hakuna neno wa si dhambi.
[Fataawaa Nuwr ‘Alad-Darb – Shariytw (34)]