035-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Twahara: Kupaka Juu Ya Vizuizi
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Twahara
035-Kupaka Juu Ya Vizuizi
Kwanza: Kupaka Juu Ya Khufu Mbili
Taarifu yake: Khufu ni viatu vya ngozi vinavyofunika visigino viwili. [Nayl Al-Awtwaar (1/241)].
Na kupaka kilugha ni kisoukomo (masdwar) cha kitenzi cha “amepaka”, nako ni kuupitisha mkono juu ya kitu kwa kuukunjua. [Al-Qaamuws Al-Muhiyt na Maqaayiys Al-Lughah].
Na kupaka juu ya khufu mbili maana yake ni kuitia umajimaji khufu maalumu katika wakati na mahala maalumu badala ya kuosha miguu miwili wakati wa kutawadha. [Ad-Durru Al-Mukhtaar].