06-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Mlango Wa Khul’
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلنِّكَاحِ
Kitabu cha Nikaah (Ndoa)
بَابُ اَلْخُلْعِ
Mlango Wa Khul’[1]
913.
عَنْ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّ اِمْرَأَةَ ثَابِتِ بْنِ قَيْسٍ أَتَتْ اَلنَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! ثَابِتُ بْنُ قَيْسٍ مَا أَعِيبُ عَلَيْهِ فِي خُلُقٍ وَلَا دِينٍ، وَلَكِنِّي أَكْرَهُ اَلْكُفْرَ فِي اَلْإِسْلَامِ، قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ " أَتَرُدِّينَ عَلَيْهِ حَدِيقَتَهُ؟ "، قَالَتْ: نَعَمْ. قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ " اِقْبَلِ اَلْحَدِيقَةَ، وَطَلِّقْهَا تَطْلِيقَةً} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ .
وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ: {وَأَمَرَهُ بِطَلَاقِهَا}
وَلِأَبِي دَاوُدَ، وَاَلتِّرْمِذِيِّ وَحَسَّنَهُ:{أَنَّ اِمْرَأَةَ ثَابِتِ بْنِ قَيْسٍ اِخْتَلَعَتْ مِنْهُ، فَجَعَلَ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عِدَّتَهَا حَيْضَةً}
وَفِي رِوَايَةِ عَمْرِوِ بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ عِنْدَ اِبْنِ مَاجَهْ: {أَنَّ ثَابِتَ بْنَ قَيْسٍ كَانَ دَمِيمًا وَأَنَّ اِمْرَأَتَهُ قَالَتْ: لَوْلَا مَخَافَةُ اَللَّهِ إِذَا دَخَلَ عَلَيَّ لَبَسَقْتُ فِي وَجْهِهِ}
وَلِأَحْمَدَ: مِنْ حَدِيثِ سَهْلِ بْنِ أَبِي حَثْمَةَ: {وَكَانَ ذَلِكَ أَوَّلَ خُلْعٍ فِي اَلْإِسْلَامِ}
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Mke wa Thaabit bin Qays[2] alimuendea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na akasema: Ee Rasuli wa Allaah! Thaabit bin Qays simtii kasoro katika tabia wala Dini lakini nachukia kukufuru nikiwa Muislamu. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akasema: “Utamrudishia shamba lake?” Akasema: Ndio. Rasuli wa Allaah akasema: (kumwambia Thaabit): “Kubali shamba lako na umuache talaka moja.” [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
Katika Riwaayah yake nyingine imesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuamrisha ampe talaka.”
Katika Riwaayah ya Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy ambayo imesema ni Hasan: “Mke wa Thaabit bin Qays alipewa talaka kwa kurudisha shamba, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akaamuru Eda yake iwe ni kipindi kimoja cha hedhi.”
Katika Riwaayah iliyo kwa Ibn Maajah kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb amepokea kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: “Thaabit bin Qays alikuwa na sura mbaya, mkewe akasema: “Lau si kwa sababu ya kumuogopa Allaah, ningalimtemea mate usoni mwakwe wakati anapoingia!”
Ahmad amepokea kutoka Hadiyth ya Sahl bin Hathmah: “Hiyo ndiyo ilikuwa Khulu’ ya kwanza katika Uislamu.”
[1] Khulu’ maana yake kilugha ni kuvua nguo. Kulingana na Shariy’ah khulu’ ina maana ya haki aliyonayo mwanamke kuvunja ndoa. Ana haki ya kuvunja ndoa baada ya kurudisha mahari. Mtu anaweza kutoa talaka akiwa na sababu za msingi. Vivyo hivyo, mwanamke naye ana haki ya kujivua (khulu’) baada ya kurejesha mahari kama ana haki ya msingi. Kulingana na ‘Ulamaa wengine, Khulu’ ni talaka, wakati wengine wakiichukulia kuwa ni kuvunja ndoa. Kuna rai tofauti kuhusu kurudisha mahari na haswa ile ya awali. Hivyo kimsingi mwanamme hawezi kudai mahari makubwa kurejeshewa zaidi ya mahari ile aliyotoa ya asili.
[2] Thaabit bin Qays Al-Ansaar Al-Khazraj alikuwa mmoja wa Maswahaba wakubwa na alikuwa ni msemaji mkuu wa Answaar na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ). Alishuhudia vita vya Uhud na vita vingine vilivyofuatia baada yake. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alimthibitishia Jannah na aliuwawa katika vita vya Al-Yamaamah.