07-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Nikaah: Mlango Wa Talaka
بُلُوغُ الْمَرام
Buluwgh Al-Maraam
كِتَابُ اَلنِّكَاحِ
Kitabu cha Nikaah (Ndoa)
بَابُ اَلطَّلَاقِ
07-Mlango Wa Talaka
914.
عَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {أَبْغَضُ اَلْحَلَالِ عِنْدَ اَللَّهِ اَلطَّلَاقُ} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ، وَابْنُ مَاجَهْ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَرَجَّحَ أَبُو حَاتِمٍ إِرْسَالَهُ
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Halali ichukizayo kwa Allaah ni talaka.”[1] [Imetolewa na Abuu Daawuwd na Ibn Maajah, na akaisahihisha Al-Haakim na Abuu Haatim anaiona kuwa ni Mursal]
915.
وَعَنِ اِبْنِ عُمَرَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا {أَنَّهُ طَلَّقَ اِمْرَأَتَهُ وَهِيَ حَائِضٌ فِي عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ فَسَأَلَ عُمَرُ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ ذَلِكَ؟ فَقَالَ: " مُرْهُ فَلْيُرَاجِعْهَا ، ثُمَّ لْيُمْسِكْهَا حَتَّى تَطْهُرَ، ثُمَّ تَحِيضَ، ثُمَّ تَطْهُرَ، ثُمَّ إِنْ شَاءَ أَمْسَكَ بَعْدُ، وَإِنْ شَاءَ طَلَّقَ بَعْدَ أَنْ يَمَسَّ، فَتِلْكَ اَلْعِدَّةُ اَلَّتِي أَمَرَ اَللَّهُ أَنْ تُطَلَّقَ لَهَا اَلنِّسَاءُ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: {مُرْهُ فَلْيُرَاجِعْهَا، ثُمَّ لْيُطَلِّقْهَا طَاهِرًا أَوْ حَامِلًا}
وَفِي رِوَايَةٍ أُخْرَى لِلْبُخَارِيِّ: {وَحُسِبَتْ عَلَيْهِ تَطْلِيقَةً}
وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: قَالَ اِبْنُ عُمَرَ: {أَمَّا أَنْتَ طَلَّقْتَهَا وَاحِدَةً أَوْ اِثْنَتَيْنِ، فَإِنَّ رَسُولَ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ أَمَرَنِي أَنْ أُرَاجِعَهَا، ثُمَّ أُمْهِلَهَا حَتَّى تَحِيضَ حَيْضَةً أُخْرَى، وَأَمَّا أَنْتَ طَلَّقْتَهَا ثَلَاثًا، فَقَدْ عَصَيْتَ رَبَّكَ فِيمَا أَمَرَكَ مِنْ طَلَاقِ اِمْرَأَتِكَ}
وَفِي رِوَايَةٍ أُخْرَى: قَالَ عَبْدُ اَللَّهِ بْنُ عُمَرَ:{فَرَدَّهَا عَلَيَّ، وَلَمْ يَرَهَا شَيْئًا، وَقَالَ: " إِذَا طَهُرَتْ فَلْيُطَلِّقْ أَوْ لِيُمْسِكْ}
Kutoka kwa Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: “Alimtaliki mkewe akiwa katika hedhi zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), ‘Umar akamuuliza Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) jambo hili. Akasema: “Muamrishe amrejee kisha akae naye mpaka atwaharike, halafu akipenda atakuwa naye, na kumuingilia. Hiyo ndiyo Eda aliyoiamrisha Allaah, wanawake waachwe namna hiyo.”[2] [Al-Bukhaariy, Muslim]
Katika Riwaayah nyengine ya Muslim inasema: “Muamrishe amrejee kisha amtaliki akiwa ni twahara au ana mimba.”
Katika Riwaayah nyengine ya Bukhaariy imesema: “…na itahesabiwa kuwa ni talaka moja.”
Katika Riwaayah nyengine ya Muslim kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Umar (alimuambia muulizaji): “Ama wewe umemtaliki talaka moja au mbili, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniamrisha nimrejee kisha niishi naye mpaka apate hedhi nyengine, kisha nimpe muda ili atwahirike, kisha nimtaliki kabla ya kumgusa (kumuingilia). Ama wewe umemuacha talaka tatu umemuasi Rabb wako katika Alivyokuamrisha kumtaliki mkeo.”
Katika Riwaayah nyengine imesema: “’Abdullaah Ibn ‘Umar (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) alisema: Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamrudisha kwangu wala hakuihisabu hiyo kuwa ni talaka. Akasema: “Atakapotwahirika umtaliki au ubaki naye (akiwa ni mkewe).”
916.
وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {كَانَ اَلطَّلَاقُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ وَأَبِي بَكْرٍ، وَسَنَتَيْنِ مِنْ خِلَافَةِ عُمَرَ، طَلَاقُ اَلثَّلَاثِ وَاحِدَةٌ، فَقَالَ عُمَرُ بْنُ اَلْخَطَّابِ: إِنَّ اَلنَّاسَ قَدْ اِسْتَعْجَلُوا فِي أَمْرٍ كَانَتْ لَهُمْ فِيهِ أَنَاةٌ، فَلَوْ أَمْضَيْنَاهُ عَلَيْهِمْ؟ فَأَمْضَاهُ عَلَيْهِمْ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa: Katika zama za Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), Abuu Bakar na miaka miwili ya mwanzo wa Ukhalifa wa ‘Umar, talaka tatu zilikuwa ni moja.[3] ‘Umar akasema: “Hakika watu wanalifanyia haraka jambo ambalo ndani yake linatakiwa upole. Itakuwa bora tukiwapitishia.” Akawapitishia. [Imetolewa na Muslim]
917.
وَعَنْ مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ:{أُخْبِرَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ عَنْ رَجُلٍ طَلَّقَ اِمْرَأَتَهُ ثَلَاثَ تَطْلِيقَاتٍ جَمِيعًا، فَقَامَ غَضْبَانَ ثُمَّ قَالَ: "أَيُلْعَبُ بِكِتَابِ اَللَّهِ تَعَالَى، وَأَنَا بَيْنَ أَظْهُرِكُمْ" حَتَّى قَامَ رَجُلٌ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اَللَّهِ! أَلَا أَقْتُلُهُ؟} رَوَاهُ النَّسَائِيُّ وَرُوَاتُهُ مُوَثَّقُونَ
Kutoka kwa Mahmuwd bin Labiyd[4] (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliambiwa kuhusu mtu aliyemtaliki mkewe talaka tatu pamoja, akasimama kwa hasira akasema: “Kitabu cha Allaah kinachezewa nami niko miongoni mwenu?” Mtu mmoja akasimama na akasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Waonaje nikamuua?” [Imetolewa na An-Nasaaiy na wapokezi wake ni madhubuti]
918.
وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {طَلَّقَ أَبُو رُكَانَةَ أُمَّ رُكَانَةَ . فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ " رَاجِعِ امْرَأَتَكَ"، فَقَالَ: إِنِّي طَلَّقْتُهَا ثَلَاثًا. قَالَ: " قَدْ عَلِمْتُ، رَاجِعْهَا} رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ
وَفِي لَفْظٍ لِأَحْمَدَ: {طَلَّقَ أَبُو رُكَانَةَ اِمْرَأَتَهُ فِي مَجْلِسٍ وَاحِدٍ ثَلَاثًا، فَحَزِنَ عَلَيْهَا، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ " فَإِنَّهَا وَاحِدَةٌ} وَفِي سَنَدِهَا اِبْنُ إِسْحَاقَ، وَفِيهِ مَقَالٌ
وَقَدْ رَوَى أَبُو دَاوُدَ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ أَحْسَنَ مِنْهُ:{أَنَّ رُكَانَةَ طَلَّقَ اِمْرَأَتَهُ سُهَيْمَةَ اَلْبَتَّةَ، فَقَالَ: "وَاَللَّهِ مَا أَرَدْتُ بِهَا إِلَّا وَاحِدَةً، فَرَدَّهَا إِلَيْهِ اَلنَّبِيُّ صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ}
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Abuu Rukaanah alimtaliki Ummu Rukaanah. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Mrudie mkeo”. Abuu Rukaanah akamuambia: “Nimemtaliki talaka tatu.” Akamuambia: “Najua mrejee (mkeo).” [Imetolewa na Abuu Daawuwd]
Katika tamshi lingine la Ahmad imesema: “Abuu Rukaanah alimtaliki mkewe talaka tatu katika kikao kimoja, halafu akahuzunika kule kumtaliki mkewe. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Hiyo ni talaka moja.” Katika Isnaad zake kuna Ibn Ishaaqa[5] ambaye ndani yake kuna maelezo.
Abuu Daawuwd amepokea kwa njia nyengine bora zaidi kuliko hiyo ikisema: “Abuu Rukaanah alimtaliki mkewe anayeitwa Suhaymah talaka isiyorudiwa akasema: “Wallaahi nimekusudia talaka moja tu.” Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamrudishia mkewe.
919.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ {ثَلَاثٌ جِدُّهنَّ جِدٌّ، وَهَزْلُهُنَّ جِدٌّ: اَلنِّكَاحُ، وَالطَّلَاقُ، وَالرَّجْعَةُ} رَوَاهُ اَلْأَرْبَعَةُ إِلَّا النَّسَائِيَّ، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
وَفِي رِوَايَةٍ لِابْنِ عَدِيٍّ مِنْ وَجْهٍ آخَرَ ضَعِيفٍ:{اَلطَّلَاقُ، وَالْعِتَاقُ، وَالنِّكَاحُ}
وَلِلْحَارِثِ اِبْنِ أَبِي أُسَامَةَ: مِنْ حَدِيثِ عُبَادَةَ بْنِ اَلصَّامِتِ رَفَعَهُ:{لَا يَجُوزُ اَللَّعِبُ فِي ثَلَاثٍ: اَلطَّلَاقُ، وَالنِّكَاحُ، وَالْعِتَاقُ، فَمَنْ قَالَهُنَّ فَقَدَ وَجَبْنَ} وَسَنَدُهُ ضَعِيفٌ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mambo matatu kweli yake ni kweli na mzaha wake ni kweli:[6] nikaah, talaka na kumrejea mke.” [Imetolewa na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa An-Nasaaiy, na akaisahihisha Al-Haakim]
Na katika Riwaayah nyengine ya Ibn ‘Adiyy imepokewa kwa njia nyengine dhaifu: “…talaka, kuacha huru na ndoa.”
Al-Haarith Ibn Abuu Usaamah amepokea kutoka katika Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit ambayo ni Marfuw’: “Haifai kufanya mchezo katika mambo matatu: talaka, ndoa na kuacha huru, atakayesema maneno hayo itakuwa imepasa.” Isnaad yake ni dhaifu.
920.
وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ عَنِ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {إِنَّ اَللَّهَ تَجَاوَزَ عَنْ أُمَّتِي مَا حَدَّثَتْ بِهِ أَنْفُسَهَا، مَا لَمْ تَعْمَلْ أَوْ تَكَلَّمْ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ
Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Allaah Amesamehe Ummah wangu wanayoyazungumza nafsini mwao maadamu hawajatenda au kuyazungumza.” [Al-Bukhaariy, Muslim]
921.
وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {إِنَّ اَللَّهَ تَعَالَى وَضَعَ عَنْ أُمَّتِي اَلْخَطَأَ، وَالنِّسْيَانَ، وَمَا اسْتُكْرِهُوا عَلَيْهِ} رَوَاهُ اِبْنُ مَاجَهْ، وَالْحَاكِمُ، وَقَالَ أَبُو حَاتِمٍ: لَا يَثْبُتُ
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kwa hakika Allaah Amewasamehe umati wangu kukosea, kusahau na walilolazimishwa.”[7] [Imetolewa na Ibn Maajah na Al-Haakim. Na akasamea Abuu Haatim kuwa ‘Haikuthibitu’
922.
وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {إِذَا حَرَّمَ اِمْرَأَتَهُ لَيْسَ بِشَيْءٍ} وَقَالَ : لَقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اَللَّهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
وَلِمُسْلِمٍ:{إِذَا حَرَّمَ اَلرَّجُلُ عَلَيْهِ اِمْرَأَتَهُ ، فَهِيَ يَمِينٌ يُكَفِّرُهَا}
Kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Mtu anapojiharamishia mkewe[8] hakuna kitu.” Na akasema: “Kwa hakika mna mfano mzuri kwa Rasuli wa Allaah.”[9] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
Na katika Riwaayah ya Muslim inasema: “Mtu anapojiharamishia mkewe hiyo ni yamini na ataitolea kafara.”
923.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا {أَنَّ اِبْنَةَ اَلْجَوْنِ لَمَّا أُدْخِلَتْ عَلَى رَسُولِ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ وَدَنَا مِنْهَا. قَالَتْ: أَعُوذُ بِاَللَّهِ مِنْكَ، قَالَ: "لَقَدْ عُذْتِ بِعَظِيمٍ، اِلْحَقِي بِأَهْلِكِ} رَوَاهُ اَلْبُخَارِيُّ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa: “Bint Al-Jawn alipoingizwa kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na akamkaribia (Amrah) alisema: “Najilinda kwa Allaah kwa sababu yako.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) akamuambia: “Kwa hakika umejilinda kwa Mtukufu. Nenda kwa jamaa zako.”[10] [Imetolewa na Al-Bukhaariy]
924.
وَعَنْ جَابِرٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {لَا طَلَاقَ إِلَّا بَعْدَ نِكَاحٍ، وَلَا عِتْقَ إِلَّا بَعْدَ مِلْكٍ} رَوَاهُ أَبُو يَعْلَى، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، وَهُوَ مَعْلُولٌ
وَأَخْرَجَ اِبْنُ مَاجَهْ: عَنِ اَلْمِسْوَرِ بْنِ مَخْرَمَةَ مِثْلَهُ، وَإِسْنَادُهُ حَسَنٌ، لَكِنَّهُ مَعْلُولٌ أَيْضًا
Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna talaka ila baada ya ndoa, wala hakuna kuacha huru ila baada ya kumiliki.”[11] [Imetolewa na Abuu Ya’laa, na akaisahihisha Al-Haakim nayo ni Ma’luwl
Ibn Maajah amepokea Hadiyth kama hii kutoka kwa Al-Miswar bin Makhramah, sanad yake ni hasan lakini bado inabaki kuwa ni Ma’luwl (yenye ‘illah iliyojificha)
925.
وَعَنْ عَمْرِو بْنِ شُعَيْبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ جَدِّهِ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ لَا نَذْرَ لِابْنِ آدَمَ فِيمَا لَا يَمْلِكُ، وَلَا عِتْقِ لَهُ فِيمَا لَا يَمْلِكُ، وَلَا طَلَاقَ لَهُ فِيمَا لَا يَمْلِكُ} أَخْرَجَهُ أَبُو دَاوُدَ وَاَلتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ، وَنُقِلَ عَنْ اَلْبُخَارِيِّ أَنَّهُ أَصَحُّ مَا وَرَدَ فِيهِ
Kutoka kwa ‘Amr bin Shu’ayb kutoka kwa baba yake naye kutoka kwa babu yake amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Hakuna nadhiri kwa mwana Aadam katika asichomiliki, wala kuacha huru (mtumwa) katika asiyemmiliki, wala kutoa talaka asiyoimiliki.” [Imetolewa na Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy na wakaisahihisha.
Imenakiliwa kutoka kwa Bukhaariy kuwa Hadiyth hii ndio sahihi zaidi iliyopokewa katika mas-ala haya.
926.
وَعَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، عَنْ اَلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ قَالَ: {رُفِعَ اَلْقَلَمُ عَنْ ثَلَاثَةٍ: عَنِ اَلنَّائِمِ حَتَّى يَسْتَيْقِظَ، وَعَنِ اَلصَّغِيرِ حَتَّى يَكْبُرَ، وَعَنِ اَلْمَجْنُونِ حَتَّى يَعْقِلَ، أَوْ يَفِيقَ} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ إِلَّا اَلتِّرْمِذِيَّ وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ
Kutoka kwa ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا) amesema kuwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Kalamu zimeinuliwa kwa watu watatu:[12] aliyelala mpaka atakapoamka, mtoto mdogo mpaka atakapobaleghe na mwenda wazimu mpaka akili itakapomrudia.” [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) isipokuwa At-Tirmidhiy, na akaisahihisha Al-Haakim
[1] Hadiyth hii ina mafundisho mengi (kama ingethibitishwa kuwa ni Swahiyh). Kuwa siyo vitu vyote vilivyokuwa halaal vinapendezesha kwa Allaah, kwa mfano talaka ni jambo la halaal lakini siyo kila mara huwa ni jambo zuri. Ni halaal kwa kuwa katika mazingira mengine jambo linakuwa gumu na mtu kulazimishwa kuacha. Katika hali kama hizo, jambo hilo linakubaliwa, kama hakuna njia nyingine. Talaka ni kitu kisichokuwa kizuri, ni jambo linalopelekea uadui na ni furaha ya shaytwaan. Maana ya talaka ni kukiacha kitu huru kishariy’ah, na kumtoa mwanamke katika kifungo cha ndoa.
[2] Hadiyth hii nayo ina mafundisho kadhaa ndani yake: 1. Ni haraam kumuacha mwanamke akiwa katika hedhi, 2. Bila ushauri wa mwanamke, mtu anaweza kubadilisha uamuzi wake, 3. Ni Bid’ah kumuacha mwanamke katika hali ya Twuhr (ni pale mwanamke anapomaliza hedhi yake) ambapo ni ruhusa kufanya tendo la ndoa, ambapo ni sawa na wakati ule wa kumuacha akiwa na hedhi. Kuna aina nne za talaka, mbili katika hizo ni halaal na mbili zingine siyo halaal. Kumuacha wakati akiwa na mimba akiwa katika hali ya Twuhr ambapo kumuingilia hakuruhusiwi ni halaal, wakati kumuacha akiwa katika hedhi katika hali ya Twuhr ambapo huruhusiwa kumuingilia talaka ni haraam. Kwa upande mwingine kuna aina tatu za talaka: (i) Ahsan (ii) Hasan (iii) Bid’ah. Ahsan ni kumuacha tu pindi anapokuwa mjamzito au wakati wa Twuhr na kuacha eda ipite (eda ni muda uliopangwa wa kusubiri baada ya mwanamke kuachwa ambapo hawezi kuolewa, inatofautiana katika hali mbali mbali). Hasan ni kuacha mara tatu, katika ya tatu, katika nyakati tatu tofauti za Twuhr. Hadi talaka mbili au tohara mbili, mtu anaweza kuvunja talaka na kuoa tena. Akishatamka talaka ya tatu hawezi kuvunja talaka wala hawezi kumuoa tena mke wake aliyemuacha kabla ya kuolewa na mtu mwingine, ambaye inabidi amuingilie na ikija kutokea akaja kumuacha baadae ndipo anaweza kumuoa au afiwe na mumewe wa pili. Bid’ah ni talaka mbili au tatu kwa mara moja, ‘Ulamaa wengi wana rai kuwa talaka inayotolewa wakati wa hedhi huhesabiwa.
[3] Ni nini hukumu ya talaka tatu zinazotolewa mara moja? Kuna rai mbali mbali za ‘Ulamaa kuhusu suala hili. 1. Talaka tatu zinazotolewa mara moja na hazina nguvu zozote kishariy’ah. 2. Talaka tatu za mara moja zinahesabiwa na mwanamke anaachika. 3. Rai ya tatu ni kuwa talaka tatu zinazotolewa wakati mmoja zinazingatiwa kuwa ni talaka moja. 4. Rai ya nne ni kuwa ikiwa mwanamke alishaingiliwa, talaka zitahesabiwa, na kama hakuingiliwa, itakuwa ni moja tu. Miongoni mwa rai hizi rai ya tatu ndiyo yenye nguvu zaidi na inayoingia akilini zaidi. Hukumu hii ndiyo iliyokuwa wakati wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), hivyo basi Abuu Rukaanah aliamrishwa kumrudia mkewe baada ya kutoa talaka tatu kwa mara moja. Ingekuwa zile talaka tatu zingehesabiwa, basi Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) asingemuamrisha kumrudia mkewe. Aina hii ya talaka inaingia katika mantiki ya watu. Kwa talaka tatu, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ameweka muda wa miezi mitatu.
[4] Mahmuwd bin Labiyd bin Abuu Rafi Al-Answaaar Al-Ash-hal. Alizaliwa katika zama za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), ni Swahaba. Abuu Haatim amesema kuwa uswahaba wake haujulikani. Ama Imaam Muslim anamuona kuwa ni miongoni mwa Taabi’iyna. Alikuwa ni miongoni mwa ‘Ulamaa, alifariki mwaka wa 96 Hijriyyah.
[5] Huyu ni Abuu ‘Abdillaah Muhammad bin Ishaaq bin Yassar Al-Mutwalibi, muachwa huru wa Qayd bin Makhrama Al-Madani ambaye alikuwa ni mtaalamu katika historia na medani ya vita wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na Maswahaba zake. Alikufa mwaka 51 Hijriyyah.
[6] Kuwa vitu hivi vinne kwa namna vilivyo havifanyiwi mzaha navyo ni: 1. Ndoa, 2. Talaka, 3. Kutengua talaka, 4. Kumuacha huru mtumwa.
[7] Hii ina maana kufikiria tu talaka bila ya kutenda hakuhesabiwi. Hii ina maana vile vile talaka inayotolewa kwa kulazimishwa sio talaka. Vivyo hivyo, ndoa ya kulazimishwa nayo si ndoa.
[8] Ikiwa mtu atamuambia mke wake kuwa hataendelea na uhusiano naye na kujiharamishia mke wake haizingatiwi kuwa ni talaka bali ni kiapo ambacho kinabidi kilipiwe fidia.
[9] Mfano wa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) hapa ni pindi alipowagomea wake zake kwa muda fulani.
[10] Aina nyingine ya talaka imewekwa wazi katika Hadiyth hii, ambayo ni 1. Ushahidi na talaka ya wazi: katika hali hii hakuna haja ya nia kulingana na maneno kuwa wazi. Ni maneno pekee yanakamilisha talaka. 2. Iwe ni moja kwa moja au kwa kuashiria: katika hali hii maneno yanakuwa kwa mafumbo, na yanaweza kuwa hayana maana ya talaka. Kwa mfano: “uko huru” au “Nenda kwa wazazi wako” n.k. maneno kama haya yanapotolewa niyyah zao zitazingatiwa lakini siyo maneno yao. Ikiwa mzungumzaji ana maana ya talaka, basi itathibiti, na ikiwa hana niyyah hiyo basi haitothibitu.
[11] Hii ina maana kuwa mtu anaweza kumuacha mwanamke aliyemuoa tu.
[12] Hii ina maana ikiwa kuna aliyetoa talaka akiwa na usingizi talaka haiswihi. Kadhalika kichaa hatoi talaka, haitozingatiwa kuwa ni talaka.