009-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Mlango Wa Swalaah: Adhana Na Iqaamah
Swahiyh Fiqh As-Sunnah
Mlango Wa Swalaah
009-Adhana Na Iqaamah
Taarifu:
[Al-Lisaan, Al-Miswbaahul Muniyr, Sharhu Muntahaa Al-Iraadaat (1/122) na Al-Mumti’i (35-36)]
Maana ya adhana kilugha ni kutangaza. Allaah Anasema:
((وَأَذِّن فِي النَّاسِ بِالْحَجِّ))
((Na tangaza kwa watu Hajj)) [Al-Hajji (27:22)]
Ama kisharia, ni kutaabudia kwa Allaah Mtukufu kwa kutangazia kuingia wakati wa Swalaah kwa utajo maalumu.
Iqaamah kilugha, ni kisoukomo cha kitenzi ((أقام)) kutokana na sentensi ya أقام الشيء , anapokinyoosha mtu kitu kikanyooka. Pia neno hili lina maana nyinginezo kama kutulia, kudhihirisha na kuita. Ama kishariah, ni kutaabudia kwa Allaah kwa ajili ya kusimama na kuswali kwa utajo maalumu.