Shaykh Fawzaan: Haijuzu Kuandika Aayah Za Suwratul-Fajr Kumtakasa Maiti

 

Haijuzu Kuandika Aayah Za Suwratul-Fajr Kumtakasa Maiti Katika Matangazo Ya Vifo

 

Shaykh Swaalih bin Fawzaan Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 “Haijuzu kuandika Aaayah amabazo watu wengi wamezoa kuziandika katika matangazo ya vifo nayo ni:

 

يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ ﴿٢٧﴾

27. (Mwema ataambiwa) “Ee nafsi iliyotua.”

 

 

ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً ﴿٢٨﴾

28. “Rejea kwa Rabb wako ukiwa umeridhika na mwenye kuridhiwa (na Allaah).

 

 

فَادْخُلِي فِي عِبَادِي ﴿٢٩﴾

29. “Basi ingia miongoni mwa waja Wangu.

 

 

وَادْخُلِي جَنَّتِي ﴿٣٠﴾

30. “Na ingia Jannah Yangu.”

 

 

Kwa sababu katika Aayah hizo mna kumtakasa maiti, na hukmu yake ni kwamba (hao wamekusudiwa kuwa ni) watu wa Jannah na hivyo haijuzu (kuwabashiria ya ghayb).”

 

[Fataawaa At-Tawhiyd Linashr Al-‘Ilm An-Naafi’ Al-Muntaqaa Min Fataawaa Ash-Shaykh Swaalih Al-Fawzaan[

 

Share