013-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuingia Msikitini
Hiswnul-Muslim
013-Du’aa Ya Kuingia Msikitini
[20]
أَعُوذُ بِاللَّهِ الْعَظِيمِ، وَبِوَجْهِهِ الْكَرِيمِ، وَسُلْطَانِهِ الْقَدِيمِ، مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ.
A’uwdhu biLLaahil ‘Adhwiym wabi Wajhihil Kariym wa Sultwaanihil qadiym minash-shaytwaanir-rajiym
Najikinga na Allaah Aliye Mtukufu na kwa Wajihi Wake Karimu na kwa utawala Wake wa kale kutokana na shaytwaan aliyeepushwa na Rehma za Allaah[1]
بِسْـمِ الله، وَالصَّلاةُ وَالسَّلامُ عَلى رَسولِ الله، اللّهُـمَّ افْتَـحْ لي أَبْوابَ رَحْمَتـِك
BismiLLaah was-swalaatu was-salaamu ‘alaa Rasuwuli-LLaah. Allaahummaftah-liy abwaaba Rahmatika
Kwa jina la Allaa na Rehma[2] na amani zimfikie Rasuli wa Allaah[3]. Ee Allaah nifungulie milango ya Rehma Yako[4]
[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah ‘Amruw bin Al-Aasw (رضي الله عنهما) imemalizikia Hadiyth:
فَإذا قَالَ ذلك، قَالَ الشَّيْطانُ: حُفِظَ مِنِّي سائر الْيَوْم
…atakaposema hivyo, shaytwaan husema: “Amehifadhiwa dhidi yangu siku nzima. - Abu Daawuwd. Angalia: Swahiyh Al-Jaami’ [4591]
[2]Ibn As-Sunniy namba [88] na ameipa daraja ya Hasan Al-Albaaniy (رحمه الله)
[3]Abu Daawuwd (1/126) na angalia: Swahiyh Al-Jaami’ (1/528)
[4]Muslim (1/494)، na katika Sunan ibn Maajah، Hadiyth ya Faatwimah (رضي الله عنها)، Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:
اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي ذُنُوبِي وَافْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِك
((Allaahumma-ghfir-liy dhunuwbiy waf-tah liy abwaaba Rahmatika – Ee Allaah Nighufurie madhambi yangu na nifungulie milango ya Rehma Zako)) na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy (رحمه الله) na ina ushahidii wa Hadiyth nyingine. Angalia: Swahiyh Ibn Maajah (1/128-129)