026-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Swalaatul-Istikhaarah
Hiswnul-Muslim
026-Du’aa Ya Swalaatul-Istikhaarah[1]
[74]
عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ : كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يُعَلِّمُنَا الاسْتِخَارَةَ فِي الأُمُورِ كُلِّهَا كَمَا يُعَلِّمُنَا السُّورَةَ مِنْ الْقُرْآنِ يَقُولُ : إذَا هَمَّ أَحَدُكُمْ بِالأَمْرِ فَلْيَرْكَعْ رَكْعَتَيْنِ مِنْ غَيْرِ الْفَرِيضَةِ ثُمَّ لِيَقُلْ
Jaabir Bin ’Abdillaah (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa akitufundisha Swalaah ya Istikhaarah kama vile anavyotufunza Suwrah ya Qur-aan, akisema: ((Akikusudia mmoja wenu kufanya jambo, aswali rakaa mbili zisizo za faradhi, kisha aseme:
اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْتَخيـرُكَ بِعِلْمِك، وَأسْتَقْـدِرُكَ بِقُـدْرَتِـك، وَأَسْـألُـكَ مِنْ فَضْـلِكَ العَظـيم، فَإِنَّـكَ تَقْـدِرُ وَلا أَقْـدِر، وَتَـعْلَـمُ وَلا أَعْلَـم، وَأَنْـتَ عَلاّمُ الغُـيوب، اللّهُـمَّ إِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ (وَيُسَـمِّي حاجته) خَـيْرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، عَاجِلِهِ و آجِلِه , فَاقْـدُرْهُ لي وَيَسِّـرْهُ لي ثـمَّ بارِكْ لي فيـه، وَإِنْ كُنْـتَ تَعْـلَمُ أَنَّ هـذا الأمْـرَ شَـرٌ لي في دينـي وَمَعـاشي وَعاقِـبَةِ أَمْـري، عَاجِلِهِ و آجِلِه فَاصْرِفْـهُ عَنّيِ وَاصْرِفْني عَنْـهُ وَاقْـدُرْ ليَ الخَـيْرَ حَيْـثُ كانَ ثُـمَّ أَرْضِـني بِـه.
Allaahumma inniy Astakhiruka bi ‘Ilmika, wa Astaqdiruka bi Qudratika, wa As-aluka min Fadhwlikal-‘Adhwiym, Fainnaka Taqdiru walaa aqdir, wa-Ta’-lam walaa a’-lam, wa-Anta ‘Allaamul-ghuyuwb. Allaahumma in Kunta Ta’-lamu anna haadhal-amra (ataje mtu hapa jambo lake) khayrul-liy fiy Diyniy wama’aashiy wa ’aaqibati amriy ‘aajilihi wa aajilihi, Faqdurhu liy wa-Yassirhu liy thumma Baarik liy fiyh. Wain Kunta Ta’-lam anna haadhal-amra sharru liy fiy Diyniy wama’aashiy wa ’aaqibati amriy ‘aajilihi wa aajilihi, Faswrifhu ‘annyi wa-Swrifniy ‘anhu waqdurliyal-khayra haythu kaana thumma Ardhwiniy bih
Ee Allaah hakika mimi nakutaka (muongozo) unichagulie kwa ujuzi Wako, na nakuomba Uniwezeshe kwa uwezo Wako, na nakuomba fadhila Zako kubwa, hakika Wewe Unaweza, nami siwezi, Nawe unajua nami sijui, Nawe ni Mjuzi wa ya ghayb. Ee Allaah, iwapo jambo hili kutokana na ujuzi Wako (utalitaja jambo lako) lina kheri na mimi katika Dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu,
katika Dunia yangu na Aakhirah yangu, basi nakuomba Uniwezeshe nilipate, na Unifanyie wepesi, kisha Unibariki. Na iwapo Unajua kwamba jambo hili ni shari kwangu katika Dini yangu na maisha yangu na mwisho wa jambo langu katika Dunia yangu na Aakhirah yangu, basi liepushe na mimi nami niepushe nalo, na nipangie jambo jengine lenye kheri nami popote lilipo, kisha niridhishe kwalo[2].
Na hajuti mwenye kumtaka Itsikhaara Allaah na akawashauri waja waumini na akajidhatiti jambo lake. Anasema Allaah (سبحانه وتعالى)
وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚ
((na washauri katika mambo. Na unapoazimia basi tawakali kwa Allaah)[3]
[1] Istikhaarah ni kuomba chaguo. Na Swalaah hii inakusudiwa mtu anapotaka kufanya jambo fulani lenye kukubalika katika Shariy’ah kama mfano kuoa, kusafiri, kuchagua kazi, kuchagua masomo ya kidunia n.k basi unamwachia Allaah (سبحانه وتعالى) Akuchagulie. Kwa maana baada ya kuiswali Swalaah hii utakavyojaaliwa kupata mwongozo basi itakuwa umeshamkabili Allaah (سبحانه وتعالى) na umetwakali Kwake.
[2] Al-Bukhaariy (7/162) [1162]
[3] Aal-‘Imraan (3:159)