027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

Hiswnul-Muslim

027-Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

www.alhidaaya.com

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

 

 

Nyiradi za asubuhi na jioni.[1] Asubuhi ni baada ya Swalaah ya Alfajiri mpaka jua kuchomoza. Na jioni ni baada ya Swalaah ya Alasiri mpaka jua kuzama. Ila baadhi ya ‘Ulamaa wamesema kuwa baada ya jua kuzama na kuendelea. 

 

الْحَمْدُ لِلَّه وَحْدَهُ وَالصًّلاَةُ وَالسَّلاَمُ عَلَى مَنْ لاَ نَبَيِّ بَعْدَهُ

 

AlhamduliLlaahi Wahdahu was-Swalaatu was-salaamu ‘alaa man-laa Nabiyyi ba’dahu

 

Himdi ni za Allaah Pekee, Rehma na amani ziwe juu ya ambaye hakuna Nabiy baada yake.

 

 

[75]

 

أَعُوذُ بِاللّهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ .

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥[2]

 

 

 

 [76]

 

Soma Suwrah zifuatazo mara tatu kila moja[3]

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم. قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾ اللَّـهُ الصَّمَدُ ﴿٢﴾ لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ ﴿٣﴾ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ ﴿٤﴾

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ ﴿١﴾ مِن شَرِّ مَا خَلَقَ ﴿٢﴾ وَمِن شَرِّ غَاسِقٍ إِذَا وَقَبَ ﴿٣﴾ وَمِن شَرِّ النَّفَّاثَاتِ فِي الْعُقَدِ ﴿٤﴾وَمِن شَرِّ حَاسِدٍ إِذَا حَسَدَ ﴿٥﴾

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ .قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ ﴿١﴾ مَلِكِ النَّاسِ ﴿٢﴾ إِلَـٰهِ النَّاسِ ﴿٣﴾ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ ﴿٤﴾ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ ﴿٥﴾ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ ﴿٦﴾

 

 

 

 [77]

أَصْـبَحْنا وَأَصْـبَحَ المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هَذا الْيَوْمِ  وَخَـيرَ ما بَعْـدَهُ، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هَذا الْيَوْمِ  وَشَرِّ ما بَعْـدَهُ، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر  

 

Aswbahnaa wa aswbahal-Mulku liLLaah wal-HamduliLlaah. Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Rabbi as-aluka khayra maa fiy haadhal yawmi wakhayra maa ba’-daahu, wa a’uwdhu bika minsharri haadhal yawmi washarri maa ba’-dahuu, Rabbi a’uwdhu bika minalkasli wasuw-il kibari, Rabbi a’uwdhu bika min ‘adhaabin finnaari wa ‘adhaabin filqabri

 

Tumeingia wakati wa asubuhi na umekuwa Ufalme ni wa Allaah,  na Himdi ni Zake Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali yakuwa Peke Yake, Hana mshirika. Ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi, na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.  Rabb wangu, nakuomba kheri ya siku ya leo, na kheri ya baada ya siku hii, na ninajikinga Kwako kutokana na shari ya siku ya leo na shari ya baada ya siku hii.  Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na uvivu, na ubaya wa uzee ubaya. Rabb wangu, najikinga Kwako kutokana na adhabu ya Moto na adhabu ya kaburi[4] 

 

Na ikiingia jioni useme: 

 

 أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المـلكُ لله وَالحَمدُ لله، لا إلهَ إلاّ اللّهُ وَحدَهُ لا شَريكَ لهُ، لهُ المُـلكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كلّ شَيءٍ قدير، رَبِّ أسْـأَلُـكَ خَـيرَ ما في هـذهِ اللَّـيْلَةِ وَخَـيرَ ما بَعْـدَهـا، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّ هـذهِ اللَّـيْلةِ وَشَرِّ ما بَعْـدَهـا، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكَسَـلِ وَسـوءِ الْكِـبَر، رَبِّ أَعـوذُبِكَ مِنْ عَـذابٍ في النّـارِ  وَعَـذابٍ في القَـبْر

Amsaynaa wa amsal-Mulku liLLaah wal-HamduliLLaahi. Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu, wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. Rabbi as-aluka khayra maa fiy haadhihil-laylati wakhayra maa ba’dahaa, wa a’uwdhu bika minsharri haadhihil-laylati washarri maa ba’dahaa, Rabbi a’uwdhu bika minalkasli wasuw-il kibari, Rabbi a’uwdhu bika min ‘adhaabin finnaari wa ‘adhaabin filqabri

 

 

[78]

اللّهُـمَّ بِكَ أَصْـبَحْنا وَبِكَ أَمْسَـينا، وَبِكَ نَحْـيا وَبِكَ نَمـوتُ وَإِلَـيْكَ النِّـشور

 

Allaahumma bika aswbahnaa wabika amsaynaa, wabika nahyaa wabika namuwtu wailaykan-nushuwr

 

Ee Allaah, Kwako (kwa neema Zako) tumeingia katika asubuhi, na Kwako (kwa neema Zako) tumeingia jioni, na kwa ajili Yako ndio tumekuwa hai, na kwa ajili Yako tutakufa, na Kwako tutafuliwa[5].

 

Na jioni useme:

 

اللّهُـمَّ بِكَ أَمْسَـينا، وَبِكَ أَصْـبَحْنا، وَبِكَ نَحْـيا، وَبِكَ نَمـوتُ وَإِلَـيْكَ المَصـير

Allaahumma bika amsaynaa wabika aswbahnaa, wabika nahyaa wabika namuwtu wailaykal-maswiyr

 

Ee Allaah, Kwako (kwa neema Zako) tumefika jioni, na Kwako (kwa neema Zako) tumefika asubuhi, na kwa ajili Yako tuko hai na kwa ajili Yako tutakufa na ni Kwako tu marejeo.

 

 

 

[79]

 

اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ .

 

Allaahumma Anta Rabbiy laa ilaaha illaa Anta Khalaqtaniy wa ana ‘abduka wa anaa ‘alaa ‘ah-dika wawa’-dika mastatwa’-tu, a’uwdhu bika minsharri maa swana’-tu, abuw-u Laka bini’-matika ‘alayya waabuw-u bidhambiy, faghfirliy fainnahu laa yaghfirudh dhunuwba illaa Anta

 

Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya  ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri  Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie  kwani hakuna wa kughufuria  madhambi ila Wewe[6]

 

Mwanamke aseme:

اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا أَمَتُكَ

Allaahumma Anta Rabbiy laa ilaaha illaa Anta Khalaqtaniy wa ana amatuka...

 

Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako mwanamke...

 

 

 

[80]

 

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَصْبَـحْتُ أَشْـهِدُك، وَأُشْـهِدُ حَمَلَـةَ عَـرْشِـك، وَمَلائِكَتِك، وَجَمـيعَ خَلْـقِك، أَنَّـكَ أَنْـتَ اللهُ لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَريكَ لَـك، وَأَنَّ ُ مُحَمّـداً عَبْـدُكَ وَرَسـولُـك [7]

 

Allaahumma inniy aswbahtu ush-hiduka wa ush-hidu hamalata ‘Arshika, wamalaaikatika wajamiy’a Khaliqika, Annaka Anta-Allaahu laa ilaaha illaa Anta Wahdaka laa shariyka Laka wa anna Muhammadan ‘Abduka wa Rasuwluka

 

Ee Allaah, hakika mimi nimefikia asubuhi nakushuhudia na nina washuhudia wabeba wa ‘Arshi yako na Malaika wako, na viumbe vyako vyote kwamba Wewe ndiye Allaah,  hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, hali ya kuwa Peke Yako Huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja Wako na ni Rasulli Wako.

 

(Useme mara 4 asubuhi na jioni)

 

 

Jioni useme:

 

 اللّهُـمَّ إِنِّـي أَمْسَيْتُ أَشْـهِدُك، وَأُشْـهِدُ حَمَلَـةَ عَـرْشِـك، وَمَلائِكَتِك، وَجَمـيعَ خَلْـقِك، أَنَّـكَ أَنْـتَ اللهُ لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ وَحْـدَكَ لا شَريكَ لَـك، وَأَنَّ ُ مُحَمّـداً عَبْـدُكَ وَرَسـولُـك  

Allaahumma inniy amsaytu ush-hiduka waush-hidu hamalata ‘Arshika, wamalaaikatika wajamiy’a khaliqika, Annaka Anta-Allaahu laa ilaaha illaa Anta Wahdaka laa shariyka Laka wa-anna Muhammadan ‘Abduka warasuwluka 

 

Ee Allaah, hakika mimi nimefikia jioni nakushuhudia na nina washuhudia wabeba wa ‘Arshi yako na Malaika wako, na viumbe vyako vyote kwamba Wewe ndiye Allaah,  hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, hali ya kuwa Peke Yako Huna mshirika, na kwamba Muhammad ni mja Wako na ni Rasuli Wako

 

 

 

 [81]

 

اللّهُـمَّ ما أَصْبَـَحَ بي مِـنْ نِعْـمَةٍ أَو بِأَحَـدٍ مِـنْ خَلْـقِك، فَمِـنْكَ وَحْـدَكَ لا شريكَ لَـك، فَلَـكَ الْحَمْـدُ وَلَـكَ الشُّكْـر[8] 

Allaahumma maa aswbaha biy min ni’-matiy aw biahadim min Khalqika faminka Wahdaka laa shariyka Laka, falakal-Hamdu walakash-shukru

 

Ee Allaah, sikuamka na neema yoyote au kati ya kiumbe Chako chochote, na neema ila inatoka Kwako hali ya kuwa peke Yako Huna mshirika, ni Zako  Himdi na ni Zako shukurani.

 

 

Jioni useme:

 

اللّهُـمَّ ما أَمْسَى بِي مِـنْ نِعْـمَةٍ أَو بِأَحَـدٍ مِـنْ خَلْـقِك، فَمِـنْكَ وَحْـدَكَ لا شريكَ لَـك، فَلَـكَ الْحَمْـدُ وَلَـكَ الشُّكْـر

Allaahumma maa amsaa biy min ni’-matiy aw biahadim min khalqika faminka Wahdaka laa shariyka Laka, falakal-Hamdu walakash-shukru

 

Ee Allaah, sikufikia jioni na neema yoyote au kati ya kiumbe Chako chochote, na neema ila inatoka Kwako hali ya kuwa peke Yako Huna mshirika, ni Zako  Himdi na ni Zako shukurani.  

 

[82]

 

اللّهُـمَّ عافِـني في بَدَنـي، اللّهُـمَّ عافِـني في سَمْـعي، اللّهُـمَّ عافِـني في بَصَـري، لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ. اللّهُـمَّ إِنّـي أَعـوذُبِكَ مِنَ الْكُـفر، وَالفَـقْر، وَأَعـوذُبِكَ مِنْ عَذابِ القَـبْر، لا إلهَ إلاّ أَنْـتَ. (ثلاثاً)

Allaahumma ‘aafiniy fiy badaniy, Allaahumma ‘aafiniy fiy sam-’iy, Allaahumma ‘aafiniy fiy baswariy, laa ilaaha illaa Anta. Allaahumma inniy a’uwdhu bika minalkufri walfaqri. Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ‘adhaabil qabri laa ilaaha illaa Anta. (mara 3)

 

Ee Allaah,   nipe afya ya mwili wangu, Ee Allaah, nipe afya ya usikizi (masikio) wangu, Ee Allaah, nipe afya ya uoni (macho) wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najikinga Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe[9].  

 

 

[83]

حَسْبِـيَ اللّهُ لا إلهَ إلاّ هُوَ عَلَـيهِ تَوَكَّـلتُ وَهُوَ رَبُّ العَرْشِ العَظـيم

 

Hasbiya-Allaahu laa ilaaha illaa Huwa ‘Alayhi tawakkaltu wa Huwa Rabbul ’Arshil ‘Adhwiym   (mara 7 asubuhi na jioni)

 

Ananitosheleza Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake Yeye nimetawakali na Yeye ni Rabb wa Arshi Tukufu[10]

 

 

[84]

اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في الدُّنْـيا وَالآخِـرَة، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ العَـفْوَ وَالعـافِـيةَ في ديني وَدُنْـيايَ وَأهْـلي وَمالـي، اللّهُـمَّ اسْتُـرْ عـوْراتي وَآمِـنْ رَوْعاتـي، اللّهُـمَّ احْفَظْـني مِن بَـينِ يَدَيَّ وَمِن خَلْفـي وَعَن يَمـيني وَعَن شِمـالي، وَمِن فَوْقـي، وَأَعـوذُ بِعَظَمَـتِكَ أَن أُغْـتالَ مِن تَحْتـي

 

Allaahumma inniy as-alukal ‘aafiyah fid-dunyaa wal Aakhirah. Allaahumma inni as-alukal ‘afwa wal ‘aafiyata fiy Diyniy wa dunyaaya, wa ahliy, wa maaliy. Allaahumma-stur ‘awraatiy, wa-aamin raw’aatiy. Allaahumma-hfadhwniy min bayni yadayya, wamin khalfiy, wa ‘an yamiyniy, wa ‘an shimaaliy, wamin fawqiy, wa a’uwdhu bi’adhwmatika an ughtaala min tahtiy

 

Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na al’-aafiyah (afya, hifadhi, amani, salama) duniani na Aakhirah.  Ee Allaah, hakika nakuomba msamaha na al’-aafiyah katika Dini na dunia yangu, na ahli wangu, na mali yangu. Ee Allaah nisitiri aibu zangu na nitulize hofu yangu. Ee Allaah, nihifadhi mbele yangu, na nyuma yangu, na kulia kwangu, na kushoto kwangu, na juu yangu, na najikinga kwa Uadhimu Wako kwa kutekwa chini yangu [11]

 

 

[85]

 

اللّهُـمَّ عالِـمَ الغَـيْبِ وَالشّـهادَةِ فاطِـرَ السّماواتِ وَالأرْضِ رَبَّ كـلِّ شَـيءٍ وَمَليـكَه، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلـهَ إِلاّ أَنْت، أَعـوذُ بِكَ مِن شَـرِّ نَفْسـي وَمِن شَـرِّ الشَّيْـطانِ وَشِـرْكِه، وَأَنْ أَقْتَـرِفَ عَلـى  نَفْسـي سوءاً أَوْ أَجُـرَّهُ إِلـى مُسْـلِم .

 

Allaahumma ‘Aalimal-ghaybi wash-shahaadah, Faatwiras-samaawati wal-ardhwi, Rabba kulli shay-in wamaliykah. Ash-hadu an laa ilaaha illaa Anta. A’uwdhu Bika minsharri nafsiy, wamin sharri shaytwaani wa shirkihi, wa an aqtarifa ‘alaa nafsiy suuw-an aw ajurrahu ilaa Muslim

 

 (Soma tena nyiradi hiyo ila kwenye neno la: ‘wa shirkihi’ useme badala yake: “wa-sharakihi”)

 

 

Ee Allaah, Mjuzi wa ghayb na yaliyowazi, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Rabb wa kila kitu na Mfalme wake. Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. Najikinga Kwako kutokana na shari ya nafsi yangu na shari ya shaytwaan na shirki yake na kujichumia uovu kwa nafsi yangu au kumletea Muislamu[12]

 

 

 [86]

بِسـمِ اللهِ الذي لا يَضُـرُّ مَعَ اسمِـهِ شَيءٌ في الأرْضِ وَلا في السّمـاءِ وَهـوَ السّمـيعُ العَلـيم (ثلاثاً)

 

BismiLLaahiLLadhiy laa yadhwuru ma’-Smihi shay-un fil-ardhwi walaa fissamaai wa Huwas-Samiy’ul ‘Aliym (mara 3)

 

Kwa jina la Allaah Ambaye hakidhuru kwa jina Lake kitu chochote kile kilicho ardhini, wala mbinguni, Naye ni Mwenye Kusikia yote daima Mjuzi wa yote daima.[13]

 

 

[87]

رَضيـتُ بِاللهِ رَبَّـاً وَبِالإسْلامِ ديـناً وَبِمُحَـمَّدٍ صَلى الله عليه وسلم  نَبِيّـاً. (ثلاثاً)

 

Radhwiytu biLLaahi Rabban wabil Islaami Diynan wabi Muhammadin Swalla-Allaahu ‘alayhi wa sallam Nabiyyaa (mara 3)

 

Nimeridhika kuwa Allaah Ndiye Rabb wangu, na Uislamu ndio Dini yangu, na Muhammad (صلى الله عليه وسلم) kuwa ni Nabiy wangu[14]

 

 

[88]

يا حَـيُّ يا قَيّـومُ بِـرَحْمَـتِكِ أَسْتَـغـيث، أَصْلِـحْ لي شَـأْنـي كُلَّـه، وَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـين

Yaa Hayyu Yaa Qayyuwm bi-Rahmatika astaghiythu, Aswlihliy sha-ani kullahu walaa takilniy ilaa nafsiy twarfata ‘aynin

 

Ee Uliye Uliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu, kwa Rehma Zako ninakuomba uniokoe, nitengenezee mambo yangu  yote, wala usiniachie  nijitegemee mambo yangu mwenyewe (pasina kunisaidia) hata kwa muda (mdogo kama muda) wa kupepesa jicho[15]

 

 

 [89]

 

أَصْبَـحْـنا وَأَصْبَـحْ المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذا الـيَوْم، فَـتْحَهُ، وَنَصْـرَهُ، وَنـورَهُ وَبَـرَكَتَـهُ، وَهُـداهُ، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَه.

Aswbahnaa wa aswbahal-Mulku liLLaahi Rabbil ‘Aalamiyn. Allaahumma inniy as-aluka khayra haadhal-yawmi fat-hahu, wanaswarahu, wanuwrahu, wabarakatahu, wahudaahu, wa a’uwdhu Bika minsharri maa fiyhi washarri maa ba’-dahu

 

Tumeingia asubuhi  na imefika asubuhi na Ufalme ni wa Allaah  Rabb wa walimwengu, Ee Allaah,  hakika mimi nakuomba kheri ya siku hii ya leo, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najikinga Kwako kutokana na shari ya kilicho ndani  ya siku hii, na shari ya baada ya siku hii[16]

 

Jioni useme:

 

أَمْسَيْـنا وَأَمْسـى المُـلكُ للهِ رَبِّ العـالَمـين، اللّهُـمَّ إِنِّـي أسْـأَلُـكَ خَـيْرَ هـذهِ اللَّـيْلَة، فَتْحَهـا، وَنَصْـرَهـا، وَنـورَهـا، وَبَـرَكَتَـهـا، وَهُـداهـا، وَأَعـوذُ بِـكَ مِـنْ شَـرِّ ما فـيهـاِ وَشَـرِّ ما بَعْـدَهـا

Amsaynaa wa amsal-Mulku liLLaah Rabbil ‘Aalamiyn. Allaahumma inniy as-aluka khayra haadhihil-laylati fat-hahaa, wanaswarahaa, wanuwrahaa, wabarakatahaa, wahudaahaa, wa a’uwudhu Bika minsharri maa fiyhaa washarri maa ba’dahaa

 

Tumeingia jioni na imefika jioni na Ufalme ni wa Allaah, Rabb walimwengu, Ee Allaah hakika mimi nakuomba kheri ya usiku huu, ufunguzi wake na nusura yake, na nuru yake na baraka yake, na uongofu wake, na najikinga kwako kutokana na shari ya kilicho ndani ya usiku huu, na shari ya baada ya usiku huu.

 

 

[90]

 

أَصْـبَحْنا علـى فِطْـرَةِ الإسْلام، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن

 

Aswbahnaa ‘alaa fitwratil-Islaami, wa ‘alaa kalimatil-ikhlaasw, wa ‘alaa Diyni Nabiyyinaa Muhammadin Swalla Allaahu ‘alayhi wasallam wa ‘alaa millati Abiynaa Ibraahiyma Haniyfan Musliman wamaa kaana minal-mushrikiyn

 

Tumeingia asubuhi na maumbile ya Kiislamu na neno la ikhlaasw na Dini ya Nabiy wetu Muhammad (صلى الله عليه وسلم), na milah (Dini) ya baba yetu Ibraahiym aliyejiengua na dini potofu akashika Dini ya haki na hali  ya kuwa  Musilamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Allaah.[17]

 

 

Jioni useme: 

 

 أَمْسَيْنا علـى فِطْـرَةِ الإسْلام، وَعَلـى كَلِـمَةِ الإخْـلاص، وَعلـى دينِ نَبِـيِّنا مُحَـمَّدٍ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم  وَعَاـى مِلَّـةِ أبينـا إِبْـراهيـمَ حَنيـفاً مُسْلِـماً وَمـا كـانَ مِنَ المُشـرِكيـن

Amsaynaa ‘alaa fitwratil-Islaami, wa ‘alaa kalimatil-ikhlaaswi, wa ‘alaa Diyni Nabiyyinaa Muhammadin Swalla-Allaahu ‘alayhi wasallam wa ‘alaa millati Abiynaa Ibraahiyma Haniyfan Musliman wamaa kaana minal-mushrikiyn

 

 

Tumeingia jioni na maumbile ya Kiislamu na neno la ikhlaasw na Dini ya Nabiywetu Muhammad (صلى الله عليه وسلم), na milah (Dini) ya baba yetu Ibraahiym aliyejiengua na Dini potofu akashika dini ya haki na hali  ya kuwa  Musilamu wala hakuwa ni mwenye kumshirikisha Allaah.

 

 

 

 [91]

سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ

Subhaana-Allaahi wa Bihamdihi (mara mia moja)

 

Utakasifu ni wa Allaah na Himdi ni Zake[18]

 

 

 [92]

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

 

Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr. (mara kumi)[19] (au mara moja ukisia uvivu)

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah  peke Yake, hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza[20]

 

 

[93]

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

 

Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr.   (mara mia atakapoamka)

 

Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah  Peke Yake, Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Mweza[21]

 

 

[94]

سُبْحـانَ اللهِ وَبِحَمْـدِهِ عَدَدَ خَلْـقِه، وَرِضـا نَفْسِـه، وَزِنَـةَ عَـرْشِـه، وَمِـدادَ كَلِمـاتِـه

 

Subhaana-Allaahi wa Bihamdihi, ’adada Khalqihi wa Ridhwaa Nafsihi, wa zinata ’Arshihi wamidaada Kalimaatih (mara 3 kila asubuhi na jioni)

 

Namtakasa Allaah (na kila sifa hasi) na namhimidi kwa idadi ya Viumbe Vyake, na kwa idadi ya vilivyoridhiwa na Nafsi Yake, na kwa uzito wa ‘Arshi Yake, na kwa wingi wa wino wa (kuandikia) Maneno Yake. [[22]

 

  

[95]

اللّهُـمَّ إِنِّـي أَسْأَلُـكَ عِلْمـاً نافِعـاً وَرِزْقـاً طَيِّـباً، وَعَمَـلاً مُتَقَـبَّلاً

Allaahumma inniy as-aluka ‘ilman naafi’an warizqan twayyiban wa ‘amalam mutaqabbalan   (asubuhi)

 

Ee Allaah, hakika nakuomba elimu yenye kunufaisha na rizki njema na amali zenye kutakabaliwa[23]

 

 

[96]

أَسْتَغْفِرُ الَّلهَ وَ أَتُوبُ إِلَيْهِ

Astaghfiru-Allaahi wa atuwbu Ilayhi (mara mia kila siku)

 

Namuomba Allaah maghfirah na natubu (narejea) Kwake[24] 

 

 

[97]

أَعُوْذُ بِكَلِماتِ اللَّهِ التَّامَّتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ

A’uwdhu bikalimaatiLLaahit-ttaammati minsharri maa khalaq (mara 3 jioni na asubuhi)

 

Najikinga kwa maneno ya Allaah yaliyotimia kutokana na shari Aliyoiumba[25]

 

 

[98]

اللّهُـمَّ صَلِّ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه، كَمـا صَلَّيْـتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم. وَبارِكْ عَلـى مُحمَّـدٍ وَعَلـى أَزْواجِـهِ وَذُرِّيَّـتِه، كَمـا بارِكْتَ عَلـى آلِ إبْراهـيم. إِنَّكَ حَمـيدٌ مَجـيد

Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammadin wa ‘alaa azwaajihi wadhurriyatihi kamaa Swallayta ‘alaa aali Ibraahiym. Wabaarik ‘alaa Muhammadin wa ‘alaa azwaajihi wadhurriyatihi kamaa Baarakta ‘alaa aali Ibraahiym. Innaka Hamiydum-Majiyd

 

Ee Allaah Mswalie Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama Ulivyowaswalia  ahli wa Ibraahiym.  Na mbariki  Muhammad, na wake zake, na kizazi chake, kama Ulivyowabariki ahli zake Ibraahiym, hakika Wewe Umesifika na Umetukuka[26]

 

 

[1]Imepokewa kutoka kwa Anas  (رضي الله عنه)amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 ((لَأَنْ أَقْعُدَ مَعَ قَوْمٍ يَذْكُرُونَ اللَّهَ تَعَالَى مِنْ صَلَاةِ الْغَدَاةِ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ أَحَبُّ إِلَيَّ مِنْ أَنْ أَعْتِقَ أَرْبَعَةً مِنْ وَلَدِ إِسْمَاعِيل ، وَلَأَنْ أَقْعُدَ مَعَ قَوْمٍ يَذْكُرُونَ اللَّهَ مِنْ صَلَاةِ الْعَصْرِ إِلَى أَنْ تَغْرُبَ الشَّمْسُ أَحَبُّ إِلَيَّ مَنْ أَنْ أَعْتِقَ أَرْبَعَةً))

 ((Kukaa pamoja na watu wanaomtaja Allaah سبحانه وتعالى  kuanzia Swalaah ya Al-Fajiri mpaka kuchomoza jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuacha huru watu wanne miongoni mwa wana wa Ismaa’iyl. Na kukaa na watu wanaomtaja Allaah  سبحانه وتعالى kuanzia baada ya Swalaah ya Alasiri mpaka kuzama jua kunapendeza zaidi kwangu mimi kuliko kuwaacha huru watu wanne)) Abu Daawuwd [3667[ na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) Swahiyh Abi Daawuwd (2/698).

 

[2]Hadiyth ya Abi bin Ka’ab (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema kuhusu Aayatul-Kursiy:

  

((مَنْ قَالَهَا حِينَ يُصٍبح أجِير مِنَ الْجِنِّ  حَتَّى يُمْسي وَمَنْ  قَالَها حِينَ يُمسي أجِير مِنْهُمْ حَتَّى يُصْبح))   

((Atakayeisoma anapoamka asubuhi itamkinga na majini mpaka itakapofika jioni. Na atakayeisoma jioni atakingwa nao mpaka asubuhi)) (Aayatul-Kursiyy - Al-Baqarah 2:255) - Al-Haakim (1/562) na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh At-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/273) [655]  

[3]Hadiyth ya ’Abdullaah bin Khubayb (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

((فمن قرأها ثلاث مرات حين يصبح وحين يمسي كفته من كل شي))

((Atakayezisoma mara tatu asubuhi na jioni  zitamtosheleza kwa kila kitu)) Abu Daawuwd (4/322) [5082], At-Tirmidhiy (5/567)[3575], na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/182)

 

[4]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘wud (رضي الله عنه) - Muslim (4/2088) [2723]

 

[5] Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - At-Tirmidhiy (5/466) [3391], na taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/142)

 

[6]Hadiyth ya Shaddaad bin ‘Aws (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

((مَنْ قَالَهَا مِنْ النَّهَارِ مُوقِنًا بِهَا فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِيَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ، وَمَنْ قَالَهَا مِنْ اللَّيْلِ وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا فَمَاتَ قَبْلَ أَنْ يُصْبِحَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ))

((Atakayesema mchana akiwa na yakini nayo, akafariki siku hiyo kabla kuingia jioni basi atakuwa mtu wa Jannah, na atakayesema usiku naye akiwa yakini nayo akafariki kabla hajafika asubuhi basi yeye ni mtu wa Jannah)) - Al-Bukhaariy (7/150) [2306]- Sayyid Al-Istighfaar:

 

[7] Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

((مَنْ قالها حين يصبح أو يمسي: أربع مرات أعتقه الله من النار))

((Atakaye yasema haya asubuhi au jioni mara nne Allaah Atamuepusha na Moto)) - Abu Daawuwd (4/317) [5069], Al-Bukhaariy katika ‘Adab Al-Mufrad [1201] An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [9] Ibn As-Sunniy [70], na ameipa daraja ya Hasan Shaykh Ibn Baaz katika Majmuw’ Al-Fataawa Isnaad ya An-Nasaaiy na Abu Daawuwd katika Nafhat Al-Akhyaar (Uk. 23). Na Ibnul-Qayyim pia ameipa daraja ya Hasan katika Zaad Al-Ma’aad.  

 

Tanbihi:  Ama baadhi ya ‘Ulamaa wamesema ni Dhwa’iyf kama Imaam Al-Albaaniy kama alivyorekodi katika Dhwa’iyf Al-Jaami Hadiyth namba [5371]. Lakini Imaam Al-Albaaniy amerekodi kwa tamshi tofauti kidogo kama ifuatavyo na akaipa daraja ya Swahiyh nayo ni Hadiyth ya Salmaan bin Farsiy (رضي الله عنه):

 

من قال : اللهمَّ إني أُشهدُك، وأُشهدُ ملائكتَك ، وحملةَ عرشِك ، وأُشهدُ من في السماواتِ ومن في الأرضِ أنك أنت اللهُ ، لا إلهَ إلا أنتَ وحدَك لا شريك لك ، و أشهدُ أنَّ محمدًا عبدُك و رسولُك ، من قالها مرةً أعتق اللهُ ثلثَه من النارِ ، و من قالها مرتيْنِ أعتق اللهُ ثلثيْهِ من النارِ ، و من قالها ثلاثًا أعتق اللهُ كلَّهُ من النارِ

 

[8]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Ghannaam (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

((مَنْ قَالَها حين يصبح فَقَدْ اَدَّى شُكر يَوْمِهِ وَمَنْ قَالَ مِثْل ذلِكَ حِينَ يُمْسي فَقَدْ أّدَّى شُكْر لَيْلَتِه))

((Atakayesema kila asubuhi atatekeleza shukurani ya siku nzima, atakayesema jioni atatekeleza shukurani ya usiku mzima)) - Abu Daawuwd (4/318) [5073], An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [7]. Ibn As-Sunniy [41], Ibn Hibbaan “Mawaarid” [2361] na isnaad yake ameipa daraja ya Hasan Ibn Baaz (رحمه الله) katika Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 24).

 

Tanbihi:  Imedhoofishwa na baadhi ya ‘Ulamaa na Shaykh Al-Albaaniy (رحمه الله) Angalia:  Al-Kalim At-Twayyib [26], Swahiyh Al-Jaami’ [5730],

 

[9]Hadiyth ya Abu Bakr (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [22], Ibn As-Sunniy [69], Al-Bukhaariy katika Adab Al-Mufrad na isnadi yake ameipa daraja ya Hasan Al-‘Allaamah Ibn Baaz (رحمه الله) katika Tuhfat Al-Akhyaaar (Uk. 26). Pia Swahiyh Abi Daawuwd (5090).

 

[10] Hadiyth ya Ummu Dardaa kutoka kwa Abuu Dardaa (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

((من قالها حين يصبح وحين يمسي سبع مرات كفاه الله ما أهمه من أمر الدنيا والآخرة))

((Atakayesema asubuhi na jioni itamtosheleza katika mambo yake yanayomtia hamu ya dunia na Aakhirah)).  Ibn As-Sunniy [71] Marfuw’aa na Abu Daawuwd Mawquwfaa (4/321), na isnadi yake ameisahihisha Shu’ayb na ‘Abdul-Qaadir Al-Arnaauwtw. Taz Zaad Al-Ma’aad (2/376) .

 

Tanbihi: Imaam Ibn Baaz (رحمه الله) amesema ni Dhwa’iyf katika Fataawa Ibn Baaz (9/294)  ila  akasema juu ya hivo ni maneno mazuri ya kutamkwa ila haikuthibiti Hadiyth hiyo.

 

[11]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Umar (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd [5074], Ibn Maajah [3871]. Taz Swahiyh ibn Maajah (2/332), Taz Swahiyh Abi Daawuwd [5074]  

 

[12]Hadiyth ya Abu Hurayrah  (رضي الله عنه) - At-Tirmidhiy [3392], Abu Daawuwd [5067], na taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/142)

 

[13]Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Afaan (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

((مَنْ قَالَها ثَلاثًا إذا أصْبَحَ وَثَلاثًا إذا أمْسَى لَمْ يَضُرُّهُ شَيْء))

((Atakayesema mara tatu asubuhi na jioni hatodhuriwa na chochote)) Abu Daawuwd (4/323) [5089, 5088]. At-Tirmidhiy (5/465) [3388], Ibn Maajah [3869], Ahmad (1/72), Taz Swahiyh Ibn Maajah (2/332), Swahiyh Abi Daawuwd (5088), Swahiyh Al-Jaami’ (5745), Majmuw’ Fataawa ibn Baaz (رحمه الله) (8/108) na isnadi yake imepewa daraja ya Hasan na Al-‘Allaamah Ibn Baaz (رحمه الله) katika Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 39)

 

[14]Hadiyth ya Thawbaan bin Bujdud (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

((مَنْ قَالَها ثَلاثًا حِينَ يُصْبحُ وَ ثَلاثًا حِينَ يُمسي كَانَ حَقًّا عَلى اللهِ أنْ يُرْضِيهِ يَوْم الْقِيَامَة))

((Atakayesema mara tatu atakapofika asubuhi na mara tatu atakapofika jioni imekuwa haki juu ya Allaah Aridhike naye Siku ya Qiyaamah)). Ahmad (4/337), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [4], Ibn As-Sunniy [68], Abu Daawuwd (4/318) [5072], At-Tirmidhiy (5/465) [3389]. Ibn Maajah. Taz Majma’ Az-Zawaaid (10/119) na ameipa daraja ya Hasan Ibn Baaz (رحمه الله) katika Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 39). Adh-Dhahabiy amesema Swahiyh. Imaam An-Nawawiy amesema Isnaad yake ni ya nguvu. Atw-Twabaraniy katika Kitaab Ad-Du’aa.

 

Tanbihi:  Imaam Al-Albaaniy ameidhoofisha katika As-Silsilah Adhw-Dhwa’iyfah [5020], Dhwa’iyf Al-Jaami’ [5735]. Ila kuna Hadiyth Swahiyh kama hiyo lakini bila ya kutajwa kuitamka mara tatu. Na pia imethibiti Hadiyth Swahiyh yenye tamshi kama hilo ambayo ni:

 

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( يَا أَبَا سَعِيدٍ مَنْ رَضِيَ بِاللَّهِ رَبًّا وَبِالإِسْلاَمِ دِينًا وَبِمُحَمَّدٍ نَبِيًّا وَجَبَتْ لَهُ الْجَنَّةُ))

Kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Ee Abaa Sa’iyd! Atakayeridhia kwamba Allaah ni Rabb na Uislamu ni Dini na Muhammad ni Nabiy, atawajibika kupata Jannah)) [Muslim]

 

 

[15]Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه) Abu Daawuwd (4/3180), At-Tirmidhiy (5/465), Al-Haakim. Taz Swahiyh At-Targhiyb (1/273), Swahiyh Al-Jaami’ [5820] Katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [4] na Ibn As-Sunniy [68], na ameipa daraja ya Hasan bin Baaz (رحمه الله) katika Tuhfat Al-Akhyaar (Uk. 39)  

 

[16] Hadiyth ya Abu Maalik Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (4/322) [5084], na isnadi yake ni Hasan kutoka kwa Shu’ayb na ‘Abdul-Qaadir Al-Arnaauwtw katika Tahqiyq Zaad Al-Ma’aad (2/273). Imaam Al-Albaaniy ameisahihisha katika Swahiyh Al-Jaami’[352].

 

 

[17]Hadiyth ya ‘Abdur-Rahmaan bin Abi Abzaa (رضي الله عنه) - Ahmad (3/406, 407) na Ibn As-Sunny katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [34]. Angalia: Swahiyh Al-Jaami’ (4/209) [4674]. Taz  Majma’ Az-Zawaaid (10/119)

 

[18]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

((مَنْ قَال حِينَ يُصْبحُ وحِينَ يُمسي ... لَمْ يأْتِ أحَد يَوْم الْقِيامَةِ بِأفْضَلِ مِمَّا جَاءَ بِهِ، إلَّا أَحد قَال مِثْل ما قال، أوْ زادَ عَلَيْهِ))

((Atakayesema mara mia asubuhi na jioni  hatofika mtu siku ya Qiyaamah aliye bora kuliko aliyesema haya ila tu aliyesema kama haya au akazidisha)) Muslim (4/2071) [2733]

 

[19]Hadiyth ya Abu ‘Ayyaash (رضي الله عنه). Imesemekana jina lake ni Zayd bin Asw-Swwamit, au Zayd bin An-Nu’maan, au jina jengine - An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [24] Hadiyth ya Abu Ayyub Al-Answaariyy (رضي الله عنه) na tamshi lake: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

 

((مَنْ قالَ إذا أصْبَحَ : لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير كانَ لَهُ عَدْل رَقَبَة مِنْ وَلَدِ إسْماعِيل، وَكُتِبَ لَهُ عَشر حَسَناتِ وَحُطَّ عَنْهُ عَشر سَيِّئات، وَرُفِعَ لَهُ عَشر دَرَجات وَكانَ فَي حِرْزِ مِنَ الشَّيْطانِ حَتَّى يُمْسِي، وَإنْ قَالَها إذا أَمْسى كَانَ لَهُ مِثْل ذلِكَ حَتَّى يُصْبِحُ))

((((Atakayesema alfajiri: Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr  itakuwa ni kama kuacha huru mtumwa katika wana wa Ismaa’iyl, na Ataandikiwa mema kumi, na atafutiwa makosa kumi, atapandishwa daraja kumi, na atakuwa katika kinga ya shaytwaan mpaka afike jioni na akisema jioni atapata kama hivyo mpaka afike asubuhi)).  Hadiyth ya Abu ‘Ayyaash (رضي الله عنه) ametaja fadhila ya kusema mara moja pia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema atakapoamka asubuhi na atakapofika jioni, atapata thawabu sawa na kuacha huru mtumwa mmoja katika wana wa Ismaa’iy, ataandikiwa mema kumi, atafutiwa maovu kumi na atapandishwa vyeo kumi na itakuwa kinga kutokana na shaytwaan mpaka atakapofika jioni)) Na angalia: Swahiyh At-Targhiyb na At-Tarhiyb (1/272) [650], na Tuhfat Al-Akhyaar ya ibn Baaz (رحمه الله) (Uk. 55) 

 

[20] Abu Daawuwd (4/319) [5077], Ibn Maajah [3867]. Ahmad (4/60) na angalia: Swahiyh At-Targhiyb na At-Tarhiyb (1/270), Swahiyh Abi Daawuwd (3/957), Swahiyh Ibn Maajah (2/331), Zaad Al-Ma’aad (2/377)

 

[21] Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema   kwa siku mara mia, basi atapata sawa na thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa mema mia moja na atafutiwa makosa mia moja, na atakuwa na kinga ya shaytwaan kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake)) Al-Bukhaariy  pamoja na Al-Fat-h, (4/95) [3293], Muslim (4/2071) [2691].

 

[22]Hadiyth ya Juwayriyyah bint Al-Haarith (رضي الله عنها)  mke wa Nabiy (صلى الله عليه وسلم) – Muslim (4/2090) [2726], Swahiyh Abi Daawuwd [1503]. Swahiyh At-Targhiyb [1574], Swahiyh Al-Jaami’ [5139], Swahiyh  Al-Adab Al-Mufrad [503].

 

[23]Hadiyth ya Ummu Salamah (رضي الله عنها) Ibn As-Sunniy katika ‘Amal Al-Yawam wal-Laylah [54], Ibn Maajah [925], Taz Swahiyh Ibn Maajah (1/152).  Majmu’a Fataawa ibn ‘Uthaymiyn (13/277), Ibn Hajar Al-Asqalaaniy katika Nataaij Al-Afkaar (2/329). Na isnadi yake ni Hasan kutoka kwa ‘Abdul-Qaadir na Shu’ayb Al-Arnaauwtw katika Tahqiyq Zaad Al-Ma’aad (2/375)

 

[24]Hadiyth ya Al-Agharr bin Yasaar Al-Muzaniy (رضي الله عنه)  - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (11/101) [6307], Muslim (4/2075) [2702], Ahmad Ad-Daarimiy. Taz Swahiyh Al-Jaami’ (944). Hadiyth imepokelewa kwa mapokezi mbali mbali na namna nyingine kama Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) katika Al-Bukhaariy kwa tamshi la Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم): ((Wa-Allaahi hakika mimi namuomba Allaah maghfirah na natubu Kwake zaidi ya mara sabiini kwa siku)) Na Allaah Anajua zaidi.

 

[25]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Ahmad (2/290), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [590], ibn As-Sunniy [68]. Angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/187), Swahiyh Ibn Maajah (92/266), Tuhfat Al-Akhyaar  (Uk. 45)  Na Taz  katika   Swahiyh Al-Jaami’ [6427] Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema mara tatu jioni hatodhuriwa na mdudu wa sumu usiku huo)

 

[26]Hadiyth ya Abu Dardaa (رضي الله عنه)  - Al-Bukhaariy pamoja na Al-Fat-h (6/4-7) [3369], Muslim (1/306) [407] na kwa tamshi lake. Na wengineo kwa mapokezi mbalimbali; Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayeniswalia  asubuhi mara kumi na jioni mara kumi, nitamuombea shifaa Siku ya Qiyaamah)). Riwaayah nyingine: ((Atakayeniswalia mara moja Allaah Atamswalia mara kumi)) Rejea Adhkaar [53, 54]

Share