036-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Anaekutana Na Adui Au Mwenye Kutawala

Hiswnul-Muslim

036-Du’aa Ya Anaekutana Na Adui Au Mwenye Kutawala

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

[126]

اللّهُـمَّ إِنا نَجْـعَلُكَ في نُحـورِهِـم، وَنَعـوذُ بِكَ مِنْ شُرورِهـمْ

 

Allaahumma innaa naj-’aluka fiy nuhuwrihim, wa na’uwdhu Bika min shuruwrihim

 

Ee Allaah,  hakika sisi tunakufanya Wewe Uwe katika vifua  vyao na tunajikinga Kwako kutokana na shari zao[1]

 

 

 

[127]

اللّهُـمَّ أَنْتَ عَضُـدي، وَأَنْتَ نَصـيري، بِكَ أَجـولُ وَبِكَ أَصـولُ وَبِك أُقـاتِل

 

Allaahumma Annta ’Adhwudiy, wa Anta Naswiyriy. Bika Ajuwlu wabika aswuulu wabika uqaatilu

 

Ee Allaah Wewe Msaidizi wangu Nawe Ndiye Mnusura wangu, Kwako ninazunguka na Kwako  ninavamia na Kwako ninapigana[2]

 

 

[128]

حَسْبُـنا اللهُ وَنِعْـمَ الوَكـيل

Hasbuna-Allaah wa Ni’-mal-Wakiyl

 

Allaah Anatutosheleza Naye ni Mbora wa kumtegemea [3]

 

 

 


[1]Hadiyth ya Abu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (2/89) [1037],   Taz Swahiyh Abi Daawuwd (1537). Ameisahihisha pia Al-Haakim na ameikubali Adh-Dhahaby (2/142).

[2]Hadiyth ya Anas bin Maalik (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (3/42) [2632], At-Tirmidhiy (5/572) [3584]na taz Swahiyh At-Tirmidhiy (3/183).

[3]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما), “Ameisema Ibraahiym (عليه السلام) alipotupwa Motoni na ameisema Muhammad (صلى الله عليه وسلم) waliposema

 

إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ ﴿١٧٣﴾

 ((Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni” (Haya) Yakawazidishia iymaan; na wakasema: “Allaah Anatutosheleza Naye ni Mbora wa kumtegemea”)) (Suwrat Aal ’Imraan 3:173) - Al-Bukhaariy (5/172) [4563]. 

 

 

Share