037-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Mwenye Kuogopa Dhulma Ya Mwenye Kutawala

Hiswnul-Muslim

037-Du’aa Ya Mwenye Kuogopa Dhulma Ya Mwenye Kutawala

www.alhidaaya.com

 

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

[129]

 

أللَّهُمَّ رَبَّ السَّمواتِ السَّبْعِ وَرَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيم، كُنْ لِي جاَراً مِنْ (فُلانِ بْنِ فُلاَنٍ) وَأَحْزَابِهِ مِنْ خَلاَئِقِكَ أَنْ يَفْرُطَ عَلَيَّ أحَدٌ مِنْهُمْ أَوْ يَطْغَى، عَزَّ جاَرُكَ وَجَلَّ ثَناَؤُكَ، وَ لاَ إِلَهَ إلاَّ أَنْتَ

 

Allaahumma Rabbas-samaawatis-sab-’i wa Rabbal-‘Arshil-‘Adhwim, kun liy jaaran min (fulani bin fulani) wa ahzaabihi min Khalaaiqika an yafrutwa ‘alayya ahadun minhum aw yatw-ghaa. ‘Azza Jaaruka, wa Jalla Thanaauka, walaa ilaaha illaa Anta

 

Ee Allaah, Rabb wa mbingu saba, na Rabb wa ‘Arshi Tukufu, kuwa Mlinzi wangu kutokana na (fulani bin fulani [taja mtu unayemhofu])  na vikosi vyake miongoni mwa viumbe Vyako, kwa kunisaliti mmoja miongoni  mwao, au kunifanyia uadui. Imeimarika madhubuti hifadhi Yako, na zimetukuka sifa Zako na hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe[1]

 

 

 

 [130]

 

الله أكْبَر، الله أعَزُّ مِنْ خَلْقِهِ جَمِيْعاً، الله أعَزُّ مِمَّا أخَافُ وَأحْذَر، أعُوذُ بِاللهِ الَّذِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ هُوَ، الْمُمْسِكِ السَّمَوَا تِ السَّبْعِ أَنْ يَقَعْنَ عَلَى الأَرْضِ ِإلاَّ بِإِذْنِهِ، مِنْ شَرِّ عَبْدِكَ (فلان) وَجُنُوْدِهِ وَأَتْبَاعِهِ وَأَشْيَاعِهِ، مِنَ اْلجِنِّ والإِنْسِ، اَلَّلهُمَّ كُنْ لِيْ جَاراً مِنْ شَرِّهِمْ، جَلَّ ثَنَاؤُكَ وَعَزَّ جَارُكَ، وَتَبَارَكَ اسْمُكَ، وَلاَ إلَهَ غَيْرُكَ

 

Allaahu Akbar, Allaahu A’azzu min Khalqihi jamiy’aa. Allaahu A’azzu mimmaa akhaafu wa ahdharu. A’uwdhu biLLaahi Alladhiy laa ilaaha illaa Huwa. Al-Mumsikis-samawaatis-sab-’i an yaqa’-na ‘alal-ardhwi illaa biidhnihi, min sharri ‘abdika (fulani - mtaje mtu unayemhofu) wa junuwdihi, wa atbaa’ihi, wa ash-yaa’ihii minal jinni wal insi. Allaahumma kunliy jaaran min sharrihim, Jalla Thanaauka, wa ‘Azza Jaaruka, wa Tabaarakas-Smuka walaa ilaaha Ghayruka [mara 3]

 

Allaah ni Mkubwa, Allaah, ni Mwenye nguvu na Mshindi kuliko viumbe Vyake vyote. Allaah ni Mwenye nguvu na Mshindi kuliko kila nikiogopacho na kujihadhari. Najikinga kwa Allaah Ambaye hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye tu Ambaye  Ameshikilia mbingu saba ili zisiangukie ardhi ila kwa idhini Yake, kutokana na shari ya mja  (fulani - mtaje mtu unayemhofu) na majeshi yake, na wanaomfuata, na wafuasi wake miongoni mwa majini na watu.  Ee Allaah, kuwa Mlinzi wangu kutokana na shari yao. Zimetukuka sifa Zako na Umehishimika ulinzi Wako na Limebarikika Jina Lako, na hapana mwabudiwa wa haki ghairi Yako[2]

 

 

[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy fiy Al-Adab Al-Mufrad [707] na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [546]. 

[2]Du’aa ya ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) - Al-Bukhaariy fiy Adabil-Mufrid [708] na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Al-Adab Al-Mufrad [546].

 

 

Share