044-Hiswnul-Muslim: Analosema Na Kupaswa Kufanya Aliyefanya Dhambi

Hiswnul-Muslim

044-Analosema Na Kupaswa Kufanya  Aliyefanya Dhambi

www.alhidaaya.com

 

Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

 

[140]

 

((Hakuna mja yeyote yule anayefanya dhambi kisha akatawadha vizuri na akaswali rakaa mbili, kisha akamtaka Allaah maghfirah ila Atamghufuria))[1] 

 

 

 

[1]Hadiyth ya Abu Bakr Asw-Swiddiyq (رضي الله عنه)  na mwisho wa Hadiyth kwamba Abu Bakr akasoma:

 

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥ أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦

Na wale ambao wanapofanya uchafu (wa aina yoyote ule) au wakajidhulumu nafsi zao, humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na wao wanajua. Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, ni wenye kudumu humo.  Uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema) [Aal-‘Imraan 3: 135-136]- Abu Daawuwd (2/86) [1521], At-Tirmidhiy (2/257) [3006, 406], na ameisahihisha Al-Albaaniy (رحمه الله) katika Swahiyh Abi Daawuwd (1/283).

 

 

Share