045-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kumfukuza Shaytwaan Na Wasiwasi Wake

Hiswnul-Muslim

045-Du’aa Ya Kumfukuza Shaytwaan Na Wasiwasi Wake

www.alhidaaya.com

 

 Bonyeza Hapa Usikilize

 

 

Mambo yafuatayo yanatakiwa kufuatwa pindi anapotolewa shaytwaan:

 

 

[141]

 

1-Omba kinga kwa Allaah Akukinge naye[1]. (useme:

أَعـوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْـطانِ الرَّجيـم

 

Au’wudhu biLLaahi minash-shaytwaanir-rajiym

 

 

 

[142]

 

2-Kuadhini  (yaani kutoa adhaana kama ya Swalaah)[2]

 

 

 

[43]

 

3-Kusoma nyiradi (zilizopokewa kutoka kwa Nabiy Muhammad صلى الله عليه وسلم)  na kusoma Qur-aan[3]

 

 

 


[1]Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa akisema anapofungua Swalaah:

أَعُوذُ بِاللهِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ مِنْ هَمْزِهِ وَنَفْخِهِ وَنَفْثِهِ

((......A’uwdhu biLLaahi minash-shaytwaanir-rajiymi min hamzihii wa nafkhihii wa nafathihi - Najilindia na Allaah kutokana na shaytwaan aliyefukuzwa, najilinda na (kutokana na) wazimu wake na kiburi chake, na ushairi [kutabana] wake)) - Abu Daawud (1/620) [771], At-Tirmidhiy (1/282) [242], Ahmad (15/81) [11472], na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (1/77). Na Allaah Anasema:

 

وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ ﴿٩٧ وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ ﴿٩٨

Na sema: “Rabb wangu! Najikinga Kwako kutokana na mnong’ono (uchochozi na wasiwasi) wa mashaytwaan,” “Na najikinga Kwako Rabb wasinihudhurie.” (Al-Mu-uminuwna 23:98-99)

 

[2]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Inapoadhiniwa kwa ajili ya Swalaah, shaytwaan hukimbia nyuma na kutoa mashuzi ili asisikie adhana. Adhana inapomalizika hugeuka. Inapokimiwa Swalaah hurudi nyuma. Inapomalizika hugeuka na kumshawishi mtu nafsi yake akisema: ”Kumbuka kadhaa! Kumbuka kadhaa” kuhusu jambo ambalo mtu hakuwa akilifikiria, mpaka hubakia mtu [amepotelewa] hajui kaswali [rakaa] ngapi)) - Al-Bukhaariy (1/151) [608], Muslim (1/291) [389],

 

[3]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Msifanye nyumba zenu makaburi. Hakika shaytwaan anakimbia nyumba inayosomwa humo Suwratul-Baqarah)) Muslim (1/539). Na mengineyo yanayomkimbiza shaytwaan ni: nyiradi za asubuhi na jioni, za kulala na kuamka, za kuingia nyumbani na kutoka, za kuingia Msikitini na kutoka humo na nyinginezo kati ya nyiradi zilizothibiti katika  Sunnah; mfano kusoma Aayatul-Kursiy wakati wa kulala, Aayah mbili za mwisho katika Suwratul-Baqarah. Na atakayesema:

 

لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

”Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr”  Mara mia itakuwa ni hifadhi kwake kutokana na shaytwaan siku yake nzima. Adhana pia inakimbiza shaytwaan kama ilivotangulia kutajwa.

 

 

Share