057-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kumtaazi (Kumhani) Aliyefiliwa
Hiswnul-Muslim
057-Du’aa Ya Kumtaazi (Kumhani) Aliyefiliwa
[162]
إِنَّ للهِ ما أَخَذ، وَلَهُ ما أَعْـطـى، وَكُـلُّ شَيءٍ عِنْـدَهُ بِأَجَلٍ مُسَـمَّى، فَلْتَصْـبِر وَلْتَحْـتسِبْ
Inna liLLaahi maa Akhadha wa-Lahu maa A’-twaa, wakullu shay-in ‘Indahu biajalin musammaa, faltaswbir waltahtasib
Kwa hakika ni Chake Allaah Alichokichukua na ni Chake Alichokitoa, na kila kitu Kwake kina muda maalum, basi vuta subira na taka malipo kwa Allaah[1]
na akisema ifuatavyo pia bora:
أَعْظَـمَ اللهُ أَجْـرَكَ، وَأَحْسَـنَ عَـزاءَ كَ، وَغَفَـرَ لِمَـيِّتِكَ
A’-dhwama-Allaahu ajrak, wa ahsana ’azaa-aka, wa ghafara limayyitika
Allaah Afanye malipo yako makubwa, na Akufanye kuzuri kutaaziwa (kuhaniwa) kwako na Amghufurie maiti wako[2]
[1]Hadiyth ya Usaamah bin Zayd (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (2/80) [1284], Muslim (2/636) [933] na katika Musnad Ahmad
[2]Al-Adhkaar, lin-Nawawy (Uk. 126)