056-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Maiti Ya Mtoto Mdogo Wakati Wa Kumswalia
Hiswnul-Muslim
056-Du’aa Ya Maiti Ya Mtoto Mdogo Wakati Wa Kumswalia
[160]
أللَّهُمَّ أَعِذْهُ مِنْ عَذابِ الْقَبْرِ
Allaahumma A’idh-hu min ’adhaabil-qabr
Ee Allaah mkinge na adhabu ya kaburi[1]
اللهُـمِّ اجْعَلْـهُ فَرَطـاً وَذُخْـراً لِوالِـدَيهِ، وَشَفـيعاً مُجَـاباً، اللهُـمِّ ثَـقِّلْ بِهِ مَوازيـنَهُما، وَأَعْـظِمْ بِهِ أُجُـورَهُـما، وَأَلْـحِقْـهُ بِصَالِـحِ الـمؤْمِنـين، وَاجْعَلْـهُ في كَفـَالَةِ إِبْـراهـيم، وَقِهِ بِرَحْمَـتِكَ عَذابَ الْجَـحِيمِ، وَأَبْـدِلْهُ داراً خَـيْراً مِنْ دارِه، وَأَهْلاً خَـيْراً مِنْ أَهْلِـه، اللَّهُمَّ اغْفِرْ لإِسْلافِنَا، وَأَفْراطِنَا وَمَنْ سَبَقَنَاَ بِالإِيمَان
Allaahummaj-’alhu faratwan wa dhukhran li waalidayhi, wa shafiy’an mujaaba. Allaahumma thaqqil bihi mawaaziynahumaa wa A’-dhwim bihi ujuwrahumaa, wa alhiq-hu biswaalihil Mu-uminiyna, waj-’alhu fiy kafaalati Ibraahiyma, waqihi Birahmatika ’adhaabal-jahiym. Wa Abdilhu daaran khayran min daarihi, wa ahlan khayran min ahlihi. Allaahumma-Ghfir li-aslaafinaa, wa afraatwinaa, waman sabaqanaa bil iymaan.
Ee Allaah Mjaaliye kuwa ni kitangulizi na akiba kwa wazazi wake na ni kiombezi chenye kukubaliwa du’aa yake. Ee Allaah kwa ajili yake Zifanye nzito mizani za wazazi wake na Yafanye mengi malipo yao, na Mkutanishe na wema wa Waumini na Mjaalie awe katika dhamana ya Ibraahiym na Muepushe kwa Rehma Yako na adhabu ya Moto, na Mbadlishie nyumba bora kuliko nyumba yake, na jamaa bora kuliko jamaa zake. Ee Allaah, waghufurie waliotangulia na waliopita na waliotutangulia katika Iymaan (Uislamu)[2]
[161]
اللهُـمِّ اجْعَلْـهُ لَنا فَرَطـاً وَسَلَـفاً وَأَجْـراً
Allaahummaj-’alhu lanaa faratwan wa salafan wa ajraa.
Ee Allaah mfanye kwetu sisi ni kitangulizi cha malipo na dhamana na malipo[3]
[1]Du’aa ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Amesema Sa’iyd bin al-Musayyib: “Niliswali nyuma ya Abu Hurayrah aliyemswalia mtoto asiyetenda dhambi kamwe nikamsikia akisema (hivyo)” Imepokewa na Maalik katika Al-Muwattwaa (1/288), Ibn Abi Shaybah katika Al-Muswannif (3/217), Al-Bayhaqiy (4/9), na isnadi yake ameisahihisha Al-Arnaawuutw katika utafiti wake ya ‘Sharh Sunnah lil-Baghawiy (5/357)
[2]Angalia: Al-Mughniy ya ibn Qudaamah (3/416) na Ad-Duruws Al-Muhimmah Li’aamatil-Ummah ya Shaykh ‘Abdil-Aziyz bin ‘Abdillaah bin Baaz (رحمه الله) (Uk 15).
[3]Du’aa ya Hasan Al-Baswry (رحمه الله), “Alikuwa Al-Hassan anamsomea mtoto mdogo Suwratul-Faatihah kisha anasema hivyo”. Al-Baghaawiy katika Sharh As-Sunnah (5/357) na ’Abdur-Razzaaq [6588] na Al-Bukhaariy ameihusisha katika Kitaab Al-Janaaiz [65] mlango wa ’Qiraat Al-Faatihaa ’Alal-Janaazah’ (2/113)