060-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuzuru Makaburi
Hiswnul-Muslim
060-Du’aa Ya Kuzuru Makaburi
السَّلامُ عَلَـيْكُمْ أَهْلَ الدِّيارِ مِنَ المؤْمِنيـنَ وَالْمُسْلِمينَ، وَإِنّا إِنْ شاءَ اللهُ بِكُـمْ لاحِقُـونَ، (وَيَرْحَمُ اللَّهُ الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنَّا وَالْمُسْتَأْخِرِينَ) أَسْـاَلُ اللهَ لَنَـا وَلَكُـمْ العَـافِيَةَ.
Assalaamu ’alaykum ahlad-diyaar minal Mu-uminiyna wal Muslimiyn, wainnaa In Shaa Allaahu bikum laahiquwn. (Wa yarhamu-Allaahu al-mustaqdimiyna minnaa wal musta-akhiriyna). As-alu-Allaaha lanaa walakumul-’aafiyah
Amani ishuke juu yenu watu wa nyumba za Waumini na Waislamu, nasi apendapo Allaah tutakutana nanyi (Na Allaah Awarehemu wa mwanzo na wa mwisho). Namuomba Allaah Atupe sisi nanyi Al-’Aafiyah[1]
[1]Hadiyth ya Buraydah bin Al-Huswayb (رضي الله عنه) - Muslim (2/671) [975], Ibn Maajah na tamshi lake (1/494) [1547]kutoka kwa Buraydah (رضي الله عنه). Yaliyo katika mabano ni Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) iliyopokelewa na Muslim (2/671) [974].
Al-‘Aafiyah: Ni neno linalojumuisha Allaah (عزّ وجلّ) kumjaalia mja Wake salama na kumpa amani, na kumlinda na maradhi, balaa, majanga, madhara, misukosuko, na kila aina za shari za wanaadam na majini na kubakia salama katika Dini yake na Aakhirah yake.