061-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Upepo Mkali
Hiswnul-Muslim
061-Du’aa Ya Upepo Mkali
[166]
اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَها، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها.
Allaahumma inniy as-aluka khayrahaa wa a’uwdhu Bika min sharrihaa
Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kheri ya upepo huu, na najikinga Kwako na shari yake[1]
[167]
اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَها، وَخَيْـرَ ما فيهـا، وَخَيْـرَ ما اُرْسِلَـتْ بِه، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها، وَشَـرِّ ما فيهـا، وَشَـرِّ ما اُرْسِلَـتْ بِه.
Allaahumma inniy as-aluka khayrahaa wakhayra maa fiyhaa, wakhayra maa ursilat bihi. Wa a’uwdhu Bika min sharrihaa, washarri maa fiyhaa washarri maa ursilat bih
Ee Allaah nakuomba kheri yake na kheri ya kilicho ndani yake, na kheri ya iliyotumwa ndani yake. Na najikinga Kwako kutokana na shari yake na shari iliyoko ndani yake na shari iliyotumwa nao[2]
[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Abu Daawuwd (4/326) [5097], Ibn Maajah (2/1228) [3727], na angalia: Swahiyh Ibn Maajah (2/305).
[2]Hadiyth ya ‘Aaishah (رضي الله عنها) - Al-Bukhaariy (4/76) [3206], Muslim (2/616) [899].