076-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuomba Unapoona Matunda Yanachipua Kwenye Miti
Hiswnul-Muslim
076-Du’aa Ya Kuomba Unapoona Matunda Yanachipua Kwenye Miti
[187]
اللّهُـمَّ بارِكْ لَنا في ثَمَـرِنا، وَبارِكْ لَنا في مَدينَتِنـا، وَبارِكْ لَنا في صَاعِنـَا، وَبارِكْ لَنا فِي مُدِّنا
Allaahumma Baarik lanaa fiy thamarinaa, wa Baarik lanaa fiy madiynatinaa. Wabaarik lanaa fiy swaa’inaa, wa Baarik lanaa fiy muddinaa
Ee Allaah Tubarikie matunda yetu, na tubarikie Mji wetu, na Tubarikie pishi (swaa’a) yetu na tubarikie kibaba (mudd) chetu[1].
[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Muslim (2/1000) [1373]
Swaa’a: Ni pishi na ni sawa na taqriban Kilo 2 1⁄2 au 3 .