077-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kupiga Chafya (Kuchemua)
Hiswnul-Muslim
077-Du’aa Ya Kupiga Chafya (Kuchemua)
[188]
Akichemua mmoja wenu aseme:
الْحَمْـدُ للهِ
AlhamduliLLaah
Himdi Anastahiki Allaah
Kisha mwenzake amwambie:
يَرْحَمُـكَ الله
Yarhamuka-Allaah
Allaah Akurehemu
Mwanamke aambiwe:
يَرْحَمُـكِ الله
YarhamukiLLaah
Kisha naye amjibu:
يَهْـديكُـمُ اللهُ وَيُصْـلِحُ بالَـكُم
Yahdiykumu-Allaahu wa Yuswlihu baalakum
Akuongoze Allaah na Akutengenezee mambo yako[1]
[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) - Al-Bukhaariy (7/125) [6224]