080-Hiswnul-Muslim: Du’aa Anayoomba Bwana Harusi Au Aliyenunuwa Kipando
Hiswnul-Muslim
080-Du’aa Anayoomba Bwana Harusi Au Aliyenunuwa Kipando
(Gari, Mnyama Na Kadhaalika)
[191]
اللّهُـمَّ إِنَّـي أَسْـأَلُـكَ خَيْـرَها، وَخَيْـرَ ما جَبَلْـتَهَـا عَلَـيْه، وَأَعـوذُ بِكَ مِنْ شَـرِّها، وَشَـرِّ ما جَبَلْـتَهَـا عَلَـيْه
Allaahumma inniy as-aluka khayrahaa, wakhayra maa jabaltahaa ’alayhi. Wa a’uwdhu Bika min sharrihaa washarri maa jabaltahaa ’alayhi.
Ee Allaah hakika mimi nakuomba kheri ya (mke) huyu na kheri ya maumbile Uliyomuumba nayo. Na najikinga Kwako na shari yake, na shari ya maumbile Uliyomuumba nayo[1].
Na ukinunua mnyama mshike kichwa chake na kisha usome du’aa hiyo
[1]Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amruw bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) , kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم):
((إِذَا تَزَوَّجَ أَحَدُكُمُ امْرَأَةً أَوِ اشْتَرَى خَادِمًا، فَلْيَقُلْ : اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ خَيْرَهَا وَخَيْرَ مَا جَبَلْتَهَا عَلَيْهِ، وَأَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّهَا وَمِنْ شَرِّ مَا جَبَلْتَهَا عَلَيْهِ، وَإِذَا اشْتَرَى بَعِيرًا فَلْيَأْخُذْ بِذِرْوَةِ سَنَامِهِ وَلْيَقُلْ مِثْلَ ذَلِكَ))
((Atakapofunga ndoa mmoja wenu au akanunua khaadimaa aseme: Ee Allaah hakika mimi nakuomba kheri ya (mke) huyu na kheri ya maumbile Uliyomuumba nayo. Na najikinga Kwako na shari yake, na shari ya maumbile Uliyomuumba nayo. Na atakaponunua mnyama amshike kichwa chake na aseme hivyo)) - Abu Daawuwd (2/248) [2160, Ibn Maajah (1/617) [1918], na taz Swahiyh Ibn Maajah (1/324).