083-Hiswnul-Muslim: Du’aa Unapomuona Aliyepatwa Na Mtihani (Kilema, Maafa Na Kadhaalika)
Hiswnul-Muslim
083-Du’aa Unapomuona Aliyepatwa Na Mtihani
(Kilema, Maafa Na Kadhaalika)
[194]
الْحَمْـدُ للهِ الّذي عافاني مِمّا ابْتَـلاكَ بِهِ، وَفَضَّلَـني عَلى كَثيـرٍ مِمَّنْ خَلَـقَ تَفْضـيلا.
AlhamduliLlaah Alladhiy ‘Aafaaniy mimmab-talakaa bihi wa fadhwalaniy ‘alaa kathiyrin mimman Khalaqa tafdhwiylaa
Himdi Anastahiki Allaah, Ambaye Ameniepusha na kile Alichokupa mtihani na Akanifanya mimi kuwa bora kuliko wengi miongoni mwa Aliowaumba[1]
[1]Hadiyth ya Abu Hurayrah (رضي الله عنه) , Kauli ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم)
((مَنْ راْ مُبْتَل فَقال: الْحَمْـدُ للهِ الّذي عافاني مِمّا ابْتَـلاكَ بِهِ، وَفَضَّلَـني عَلى كَثيـرٍ مِمَّنْ خَلَـقَ تَفْضـيلا، لَمْ يُصِبْهُ ذالك الْبَلاء))
((Atakayemuona aliyepatwa na mtihani akasema: Himdi ni za Allaah, Ambaye Ameniepusha na kile Alichokupa mtihani na Akanifanya mimi kuwa bora kuliko wengi miongoni mwa Aliowaumba, hatofikwa na mtihani huo)) - At-Tirmidhiy (5/493-4), Ibn Maajah. Angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/153)