084-Hiswnul-Muslim: Du’aa Ya Kuomba Katika Kikao
Hiswnul-Muslim
084-Du’aa Ya Kuomba Katika Kikao
[195]
عَنْ ابْنِ عُمَرَ (رضي الله عنهما) قَالَ: كَانَ يُعَدُّ لِرَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي الْمَجْلِسِ الْوَاحِدِ مِائَةُ مَرَّةٍ مِنْ قَبْلِ أَنْ يَقُومَ:
Imepokewa kutoka kwa Ibn ’Umar (رضي الله عنهما) ambaye amesema: ”Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) alikuwa aksioma mara mia moja du’aa hii kabla hajasimama katika kikao chake kimoja:
رَبِّ اغْفِـرْ لي، وَتُبْ عَلَـيَّ، إِنَّكَ أَنْـتَ التَّـوّابُ الغَـفُورُ
Rabbi-Ghfir liy wa tub ’alayya Innaka Antat-Tawwabul Ghafuwr
Allaah Nighufurie na Nikubalie toba yangu, hakika Wewe ni Mwingi wa Kupokea tawbah, Mwingi wa kughufuria[1]
[1]At-Tirmidhiy [3432] na wengineo na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (3/153) na Swahiyh Ibn Maajah (2/321) na tamshi la At-Tirmidhiy.